KUTOKWA MACHOZI WAKATI WA KUKATA KITUNGUU.

KUTOKWA MACHOZI WAKATI WA KUKATA KITUNGUU.
Kwa Wale Waliowahi Kukata Vitunguu Watakuwa Wanafaham Hii Tabu Ya Kutokwa Machoz Wakat Wa Kukatakata Vitunguu 😂😂😂 Wale Wa Jikon Kila Siku Poleni Na Mimi Wa Kachumbari Pole Pia .
Sasa Ipo Hivi Kitunguu Huwa Kina Sulfur ambayo Huwa Inakipatia Kitunguu Kale Ka Ladha Kake lakini pia Huwa Ina enzyme (Kimeng'enya)Fulani Ndani Yake, Unapoanza Kukata Kitunguu Hicho Kimeng'enya Huwa Kinatoa Kemikali Inayoitwa Propanethila S-Oxide Na kemikali Hii Hutengeneza Gesi Ambayo Huanza Kusambaa Kweny Hewa Na Kuja Kweny Macho yako Sasa Inapofika Kweny Macho Huwa Kuna Vifuko Vya Kutengeneza machoz Vinaitwa Lacrimal Gland(Zipo Pembni Karib na Pua kweny pembe ya karb na Pua) . Inapofika Hapo Na Kuingia Inatengeneza Muwashoo Baadae Machozi Yanatoka Sabab Ya Muwasho Ule.
Unaweza Kuepuka Kutokwa na machozi Ukiwa unakatakata Vitunguu Mfano Wa njia Nyepesii Ni Kama; ●Kufaa Miwan Maalumu za Kupikia, Hizi Zitazuia Gesi Ile Isiweze Kuingia Machoni na Kukuwasha. ●Kuwa na mazoea ya Kutunza Vitunguu kweny Frijii maana Ubarid huwa unapunguza Kemikali ile. Maana Mazingira Ya Joto Yanachochea Kemikali Hio. ●Tumia Feni Wakat wa kukata Vitunguu Hii itasaidia Kuepuka gesi Ile Kwa Kupigwa na upepo Hivyo huepuka Kuingia machoni. ●Ukishindwa Basi Kata vitunguu umeinua Kichwa Juu Hata Pia Tafuna Jojo huku unakata 😂😂😂. MWISHO

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages