BINADAMU WA BLUE (Blue man)
Paul Karason alizaliwa akiwa na ngozi yenye rangi ya kawaida.Baada ya kuugua magonjwa ya ngozi kwa muda mrefu,aliamua aanze kujitibu kwa kutumia kemikali za colloidal silver.Ilipita miaka 6 baadae ndipo ngozi yake ilipobadilika na kuwa ya rangi ya blue,tatizo linalojulikana kama Argyria.Muingreza huyu anajulikana sana kama "binadamu wa blue".Alifariki akiwa na miaka 62 baada ya kupatwa na shambulio la moyo pamoja na kiharusi
.
LENGO LA HADITHI HII FUPI
Lengo la hadithi hii ni kutoa tahadhari kwa dawa tunazotumia kila siku bila kupima,kwa kukariri,mazoea au kwa kusikia tu kuwa dawa fulani hutibu tatizo ulilonalo kwa wakati huo.Dawa inaweza ikawa sumu na kuyabadilisha kabisa maisha yako ndani ya muda mfupi.USITUMIE dawa yoyote bila kuwa na maelezo yake sahihi,na ikitokea umenunua dawa kisha ukasahau matumizi yake USIINYWE,rudi ulikoichukulia upewe maekezo yake.Mambo haya yote yakishindikana basi itupe kabisa.Matatizo yanaweza yasitokee kwako moja kwa moja lakini yakaja kutokea kwa vizazi vyako.Chukua tahadhari leo
BINADAMU WA BLUE (Blue man)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment