Huyu alizaliwa mwaka, 1946, Nchini ufaransa na kufa mwaka 1993, paris ufaransa.
Huyu mtu, alikuwa anaongezeka Ukubwa haraka sana, kinyume na inavyotakiwa.. kwasababu alizaliwa akiwa na tatizo la Gigantism(Giantsim), yan ni matokeo ya homoni za ukuaji kuzalishwa kwa wingi sana kupita kihasi stahiki.
Sasa ili tatizo, lilimpelekea andrew kukua kwa haraka sana,..unambiwa kipindi alipo kuwa na miaka 12, tayari alikuwa na urefu wa ft 6.3.
Baada ya kuona maumbile yake tofaut aliamua kuacha shule na kufanya shughuli za nyumbani, ambapo kaka yake Jaque, alisema, andrew alikuwa na nguvu sana kiasi cha kufanya kazi za watu wa tatu pekeyake.
Alipo fikisha miaka 14, andrew ali ondoka nyumbani na kwenda kutafuta maisha, ambapo huko alienda kujifunza mieleka kutokana na umbo lake, na alipata umaharufu na kuanza kupigana katika matamasha mbali mbali ufaransa.
Wakati huo endrew anapigana mieleka , wazazi wake haswa baba yake siku zote walikuwa wakiangalia mchezo huo, lakini hawakutambua kama ni andrew mtoto wao kwasababu alikuwa anakuwa haraka sana kimaumbile, na baba yake alinukuliwa akisema alikuwa nishabiki wa andrew, lakini alikuwa hajui kama anamshabikia mwanae.
Andrew alipofikisha miaka 19, alirudi nyumbani ndipo wazazi na familia kwa ujumla walipo staajabika hususani baba yake baada ya kujua kumbe ana mshabikia mwanae.
Bada ya apo aliamia japan na kisha Marekani ambapo huko ndipo alipo pata umaarufu, baada ya kujiunga na WWF(WWE kwa sasa), ni kampuni kubwa ya mchezo wa mieleka duniani.
Pia andrew anashikilia record ya kuwa ndie mtu anaekunywa pombe nyingi duniani, hayo yaliongewa na marafiki wake wa karibu akiwemo Anord schwazniger, ambae alisema haku amini siku waliokuwa kwenye baa, na kumwona Andrew akinywa vyupa vya bia 127.
Unaambiwa alikuwa ana uwezo wa kunywa bia ,lita 41, kwa saa 6..Andrew alikufa kwa ugonjwa wa moyo, alikuwa na urefu wa ft 7.4, na uzito wa kg 200, na ujazo wa 500 pound.
Aliacha historia katika mchezo wa mieleka WWE, kwasababu ndie mtu alie upa mchezo huo umaarufu, kihasi kwa kuwa na heshima kubwa katika mchezo huo, na wana muenzi kila mwaka, ambapo lilianzishwa pambano la Royalrumble match katika westlemania 34.

No comments:
Post a Comment