Unju Bin Unuq (jitu kubwa)

Unju Bin Unuq anasemekana alikuwa ni Jitu Kubwa, Refu alikuwa na Maajabu Kadhaa Kama Urefu Wake Ambapo Inasemekana Kwake Baharini Maji Yalikuwa Yakimfika Magotini Na Hapo Akiwa Kakanyaga Chini Ya Bahari.
Unju bin Unuq (pia: Unju bin Unuku ,
Unzi Bin Ununuk) ni jina la jitu katika masimulizi ya wakazi wa pwani ya
Tanzania . Hadithi zake zasimuliwa kuanzia Bagamoyo hadi Kilwa .
Historia yake inapatikana katika makumbusho ya Kaole huko Bagamoyo.
Moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni urefu wake yaani kimo , inasadikiwa alikuwa na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee baharini na miguu yake kugusa chini.
Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa moja kati ya nyayo zake inapatikana kwenye jiwe alilokanyaga huko Tabora , Tanzania,
wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko Kongo .
Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika jua kisha anakula.
Kuhusu maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na umbo lake.
Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju bin Unuq, aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana kidole chake chenye urefu wa kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi mwili wake uliobaki uliangukia wapi.
Unju bin Unuq alikuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya Dodoma . Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi ndugu zake wa mbali sana wameonekana katika
mkoa wa Dodoma .
Maajabu Mengine Ya Unju Bin Unuq.
* Inasimuliwa akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika Jua kisha anakula.
*Alikua akitembea kutoka nchi moja kwenda nyingine. Kuna nyayo yake ya mguu wa Kushoto inapatikana katika jiwe huko Tabora na Kulia inapatikana Congo.
* Baada ya Kufariki inaelezwa Mwili wake ulikatika vipande vipande, inaelezwa Kidole chake chenye urefu wa kilomita 1 ndicho kilipatikana na kuzikwa huko Bagamoyo.
N.b story hazina uhakika !!

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages