ERNESTO CHE GUEVARA 01

Ernesto Rafael Guevara de la Serna au Che Guevara alizaliwa jijini Rosario , Argentina , 14 Mei 1928; alikuwa tabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi wa
itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx .

Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko
Amerika ya Kusini na Afrika.

Guevara alipewa jina la "che" huko Amerika ya Kati likimaanisha "mshangao". Alitumia usafiri wa pikipiki kutoka Amerika ya Kusini hadi Amerika ya kati.

Guevara kwa sababu ya kufiwa na bibi yake aliyemuuguza kwa muda mrefu aliamua kusomea utabibu.
Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umaskini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha ya
ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi, huku wachache wakiwa wanamiliki mali za nchi hizo. •

Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa umaskini na ukandamizaji ni mapinduzi. Aliamua kusoma kwa undani falsafa ya Karl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za kisoshalisti nchini Guatemala chini ya rais Jacobo Arbenzi Guzmán .
Mwisho mwa miaka ya 1950, Guevara aliungana na Fidel Castro aliyekuwa akiongoza kundi la kijeshi lililotwaa madaraka kwa nguvu nchini
Cuba mwaka 1959. Guevara alikuwa mmoja wa viongozi wa serikali mpya ya Cuba.

Katika kipindi hiki, Guevara aliandika vitabu na makala mbalimbali kuhusu nadharia na vitendo vya vita vya msituni kwa nia ya kuondoa madarakani tawala za kibepari na kibeberu.

Itaendelea

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages