DR. CARL TANZLER......

Bwana Huyu Alizaliwa February 8 ya Mwaka 1877 huko Ujerumani . Alikua Ni Daktari mtaalamu wa Maswala Ya Picha Na Mwanga lakini pia Mwanateknolojia Katika Hospital Ya Marine. Alifanya Kaz hapo kwa Miaka Mingi kama Daktari Kweny mambo Ya X-ray.

Mwaka 1930 mwez wa Tatu akiwa anaendelea na Kazi zake Mmama Mmoja alimleta Mwanae Hospitalii Na jamaa alitokea Kumpenda Sana Yule Binti aliyejulikana Kwa Jina La Elena ama Helen . Dr tanzler Alijitolea Kumtibia Binti Yule maara Baada Ya Kugundulika Ana Kifuakikuu (TB) Aligundua Baada Ya Kufanya X-ray  Hivyo Alianza mara Moja Kumtibu Kwa Antibayotiki.

Inadaiwa Daktari Huyu alikua Akimpelekea Vijizawad Bibie Huyo kama Nguo na mapambo mbalimbali Lakini Baadae Binti Huyu alifariki baada Ya Kuzidiwa na KifuaKikuu na taratibu za mazishi Zilifuatia.

Baada Ya miaka kama Miwili Daktari Huyu hakuridhika kabisa ikiwa ni mwaka 1933 Jamaa alikwenda Kufukua kaburi la Bibie Huyo na Kubomoa na Kuutoa Mwili Wa Mwanamke Huyo na Kuamua Kuishi Nao Ndani kwakua Mwili ulikua umeshaharibika Alitumia ustadi Mkubwa  Kufunga Mifupa Na Waya , kichwani alinunua Wigi Nzuri na Kulipachika, machoni alitumia glass , kuhusu mwilii alitumia P.O.P (Plaster of paris) Kufunika Baadhi Ya sehemu Alikua anapulizia Na Marashii Mbalimbali Kukata Harufu .

Mwaka 1940 ikiwa Ni miaka takriban saba (7) akiwa anaishi na Mwili Ule Wa Binti aliyempenda Dada Yake na Marwhemu Alisikia Taarifa za Daktari Huyu Kuishii Na Mwili Wa Marehem Mdogowake . Baadae alitoa taarifa na Jamaa alikamatwa baada ya Kuvamiwa gafla na Kuukuta Mwili huo ndani jamaa alishitakiwa kwa kufukua kaburi bila ruhusa na Baadae aliachiwa. 

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages