- Raymond Robinson alizaliwa october 29, 1910 sehem mmoja huko U.S inayoitwa pennyslyvania .Kipindi akiwa mtoto akiwa na umri wa miaka 9 alipata ajali na kuunguzwa vibaya mno katika uso wake. Aliungua akiwa akipanda katika daraja moja huko lililokua na line za umeme mkubwa na mara baada ya kufika juu, huko juu ya daraja alikua anafata kiota cha ndege ndipo akapata ajali hiyo mbaya ya kuunguzwa na umeme.Bwana robinson aliishi lakin sura yake ilikua haitamaniki kabisa kwani alipoteza macho yake , pua na mkono wake wa kulia ,Muda wote huo alikua akiishi na ndugu zake huko koppel akitengeneza pochi na mikanda kwaajili ya kuuza.Muda mwingi alikua hapend kutembea wakat wa mchana kutokana na sura yake hio na alikua akitoka mchana kwa nadra sana alifanya hivo kwa kuogopa kuwatisha watu atakao kutana nao wakati wa mchana.Alipendelea kutoka nyakati za usiku na kwenda kutembea akipata sapot kwa kutumia fimbo yake.Watu mbalimbali walipenda saana kutembelea maeneo karibu na barabara ambako anaishi bwana huyo ili angalau wapate kumuona na kusimulia huko waendako.Kutokana na sura yake hio watu walimpachika jina la charlie no face au green man.Safari za bwana Robinson za kutembea usiku zilimuwia ngumu mara baada ya mara kadhaa kukoswa koswa kugongwa na magarii na aliamua kuacha kutembea usiku kabisa baada ya kuona maisha yapo hatarini .Akaamua kwenda sehem moja hivi ya kulelea wazee iitwayo Beaver County Getiatric Centre ambapo mnamo June 11 mwaka 1985 alifariki akiwa na umri wa miaka 74.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment