Capybara (Ngekewa) ni jamii ya wanyama aina ya Panya, lakini kwao ni tofauti kidogo sababu wao ni Wakubwa kiumbo tofauti na Jamii nyingi za Panya.
Ngekewa ni mojawapo ya Wanyama ambao ni wakarimu sana, hawana noma na mtu yeyote, Na jambo kidogo la Kushangazwa ni kuwa hawa ni Wanyama ambao mara kadhaa wameonekana wakiwa wamekaa pamoja na wanyama hatari bila shida yoyote, Kama Mamba.
Pia ndege kadhaa wanapenda sana kukaa Juu yao, huku Nyani nao mara kadhaa wameonekana wakipenda kucheza nao.
Ngekewa wanapatikana kwa Wingi sana Amerika ya Kusini, na Wanakaa maeneo ambayo yana maji.
Wana uwezo wa Kukaa ndani ya Maji kwa Dakika 5 bila kuibuka Juu hasa hufanya hivyo kama wakiona Hatari...lakini Pia wanaweza kukaa tu ndani ya maji kisha Huweka Pua yao juu na kupumua huku wakiwa katika Maji mara nyingi hufanya hivyo kama kukiwa na Joto kali mchana.
Hawa bila maji hawaendi sababu ya Namna ya manyoya yao kama yatapigwa na Jua kwa kiasi Fulani huanza Kuungua...hivyo mara kwa mara hutumia Maji kama kujiweka sawa na miili yao.
Ngekewa huishi kima Kundi kundi, Kuanzia 7 mpaka 15..na huongozwa na Dume mmoja...Dume ana kazi kubwa ya kutoa ulinzi kwa Kundi lake, ana uwezo mzuri wa kuona na Kuhisi Hatari...Hivyo akiona hali si shwari huwataarifu wenzake Kwa kubweka mithili kama ya Mbwa.
Miguu yao kama Bata, sababu ina Utando hiyo huwasaidia kuogelea Katika Maji na Kukeep Balance wakiwa majini lakini pia Huwawezesha kutembea hata sehemu za Michanga bila tatizo.
Ngekewa kama Kuku, hawa hata waende wapi kutafuta chakula, lakini bado watarudi nyumbani tu. Wanatumia harufu wanayoacha ya miguu yao kuifuata na kurudi nyumbani.
Hao ndio Ngekewa, Ukiambiwa Una Ngekewa Ina maana una bahati nzuri sana...na imetokana na Huyu mnyama ambae anapendwa na Wanyama hatari.
Haifahamiki Kwanini anapendwa na Wanyama wenzake.
No comments:
Post a Comment