REINCARNATION


REINCARNATION huu mchakato wa kuzaliwa tena katika umbo la kiumbe hai kingine au Binadamu kutokana na matendo yako ya nyuma baada ya kufa. Hii wanaitumia sana watu wasioamini katika Mungu mmoja bali miungu.
Kwao hakuna neno MSAMAHA. ukitenda baya utalipwa baya. Ukitenda jema utalipwa jema. Na hii hutokea ukiwa hai au ukimaliza tena.
REBIRTH ni mchakato wa kuzaliwa mara ya PILI lakini katika mwili ule ule ila likiwa ni tendo la kiroho zaidi.
Hii hutumiwa sana na waamini wanaoamini katika Mungu mmoja na maisha ya peponi baada ya kifo kama ukitubu na maisha ya jehanum kama usipo tubu na kuungama madhambi yako, Rebirth ni tendo la kuokoka kiroho.
Yote kwa yote kuna mstari mwembamba sana kati ya tafsiri hizi mbili rebirth na reincarnation. Moja ikiwa ni kuzaliwa tena na nyingine ikiwa ni kuzaliwa mara ya pili.
Moja ikiwa ni tendo la kiroho zaidi na nyingine ikiwa ni tendo la kimwili pamoja na kiroho Mfanano wao ni kwamba zote ni imani,
Kuna usemi maarufu duniani kuwa dunia wawili wawili Kwamba kuna watu wa kaliba tofauti kabisa Nchi tofauti kabisa au maeneo tofauti kabisa lakini wamefanana kama mayai.
Naamini umeshawahi kusikia mtu akikwambia kuwa nimemuona mtu anafanana na wewe kabisa Hii inaitwa living reincarnation
Swala la matunzo ya watoto waliotelekezwa na wazazi wa kiume pamoja na kwamba limekuwa la kisiasa zaidi.
Lakini kiroho lina tafsiri yake pana sana Tafsiri ya kwamba hapa duniani sura yako si yako pekee mtatofautiana vingine kama kabila umri eneo nk lakini sura ni ile ile.
Kitendo kilichofanywa na baadhi kutaka kuthibitisha madai yao ni kuweka sura za watoto na wababa wanao tuhumiwa kuwa hao ni watoto wao.
Kuna Ushahidi Kuhusu watu Mbali Mbali kufa na Kuzaliwa Wakiwa na sura zile zile na Kuuliza Maswali Ambayo Yana mahusiano na Mtu Fulani Aliye Kufa.
Itaendelea

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages