》》Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini
kuwa ngozi angavu huashiria uzuri , utajiri na
uwezo( kifedha) alionao mtu . Katika baadhi ya
sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa
kuwa wapo chini ya kiwango,
hii hupelekea watu hawa kutumia ving ´arisha ngozi
kama krimu , vidonge au nyenzo zingine
kubadilisha ngozi zao .
Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana
hupendelea kutumia bidhaa zinazong ´arisha ngozi
ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la
familia zao , na jamii . Kwa kweli , hata matangazo
yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali
huonyesha kitu hiki . Mambo hayo yote huwa na
athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na
wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague
chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge .
》》Madhara ya kujichubua ni yapi ?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa yangozi,
chunusi ,
uvimbe katika ngozi,
ngozi kuwanyembamba, Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,
kutokwa na mabaka ,
pumu ,
Kupungua kwa nuru ya macho,
kupata watoto wenye kasoro,
kupata matatizo ya akili,
kuharibika kwa ini ,
kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki
( mercury) kilichomo katika krimu , Osteoporosis
(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza
hatari ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na
mengine hujitokeza kadri mtu anavyozidi kutumia ving´arisha ngozi.
No comments:
Post a Comment