Jinsi ya kutibu ugonjwa wa mafua (Natural Way)

Karibu tena kwenye Imatheboy blog Kipindi ni Afya Topic ni kuhusu Mafua

》》Mafua pia yanajulikana kama nasopharyngitis, rhinopharyngitis, mafua ya kuku, au mafua.
-Ni ugonjwa unaoambukiza kirahisi sehemu ya juu ya mfumo wa kupumua ambao huathiri zaidi pua. Dalili ni pamoja na kikohozi, koo, ama mafua (rhinorrhea), na homa.

-Dalili kwa kawaida hutokea na kupotea baada ya siku saba hadi kumi. Ingawa baadhi ya dalili zake zinaweza zikakaa hadi wiki tatu. Kuna zaidi ya virusi mia mbili wanoweza kusababisha mafua ya kawaida. Virusi jamii ya rhinovirus ndio vinasababishi vikuu.

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa mafua
~Mafua ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza hutokea mabadiliko ya kimwili ikiwemo sehemu za viungio vya mwili kama miguu, mikono na sehemu zingine.

》》Hizi ni baadhi ya njia za kawaida zinazoweza kusaidia kukutibu kiasili:

~Ulaji wa machungwa
Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Inashauriwa kuwa ila unapokua machungwa basi hakikisha kuwa unakula na pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.

~Maziwa ya Mtindi:
Unywaji wa maziwa ya mtindi ni moja ya njia inayosaidia kupunguza ugonjwa huo, hii ni kutokana na kuwa maziwa hayo yana kiwango kikubwa cha protini na mtu mwenye mafua hupunguza kukohoa kwa kunywa maziwa hayo.

~Asali na Tangawizi:
Asali ni dawa kubwa sana ya magonjwa mbalimbali, ila ukichanganya asali na tangawizi husaidia kutibu mafua na kifua, hii ni dawa nzuri sana kwani haina madhara yoyote unaweza kutumia kwa kuiramba ama kwa kuichanganya katika chai.

~Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuw na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa makamasi. Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza sup ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.

~Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya allicin' ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua. Tumia kitunguu hicho kwa kupik kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.

~Chai, hasa ya kijani, (green tea) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal of the America College of Nutrition) umeonesha kuwa watu wanaotumia chai kwa mpangilio maalum hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kw asilimia 36 ukilinganisha na wale wasiokuwa na kinga imara.

~Wataalamu wanakubaliana kuwa ulaji wa chokoleti nyeusi (dark chocolate) huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine. Halikadhalik huwa kinga kwa maambukizi mengine.

~Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bakteria pamoja na virusi vya mafua. Kiasi kidog cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kuimarisha kinga ya mwili.

~Kirutubisho aina ya Beta-carotene' huimarisha kinga ya mwili. Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini n kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai, (kiini).

~Kwa ujumla, suala la kuimarisha kinga y mwili ni muhimu kwa afya zetu. Ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu na vingine unatakiwa kuwa ni wa mara kwa mara kama siyo wa kudumu, kwa sababu mwi unapokosa kinga imara, ni rahisi kushambuliwa na maradhi ya kuambukiza


Mambo madogomadogo ya Kuzingatia wakati unaumwa homa ya mafua

~Usikae kwenye vumbi

~Usikae kwenye moshi

~punguza mawazo yaani uwe mwenye furaha

~Nawa uso na penga makamasi kadri ya uwezavyo

~kaa sehemu yenye kivuli na hewa safi

~kunywa maji mengi 

~usitumie mafuta,lotion,sabuni wala Pafyumu zenye harufu kali 

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages