Historia ya SKULLS AND BONES

SKULLS AND BONES
-
Leo Ebu Tuwa kodolee Macho kidogo Wazee wa mafuvu na Mifupa,
Tarehe 10 February mwaka 2017 ilikuwa ni siku ya kutimiza miaka 100 tangu kifo cha Geronimo ambaye alikuwa ni shujaa kutoka Jamii ya APACHE (hawa ni mashujaa wa wahindi wekundu au wakazi asilia wa Taifa la marekani maarufu kama Red Indians). -
Ndugu mmoja katika jamii hii alifungua mashtaka akiwashtaki Skull and bones jamii ya Siri ambayo ilianzia Katika chuo kikuu cha YALE huko marekani kuwa iruhusika na kuiba mabaki ya Shujaa Geronimo.
Miaka kadhaa imekuwa ikipigiwa kelele jamii hii ya Fuvu na Mifupa kuwa imeshikilia mabaki ya Geronimo ikiyatumia kwa shughuli zake za kiimani.
-
Haryln Geronimo (Kitukuu cha Shujaa Geronimo) mwenye miaka 61 anasema “naamini kabisa toka moyoni mwangu kuwa roho ya Geronimo haikuachiliwa” akiwaambia waandishi wa habari walio kusanyika wakifuatilia tukio hili lililo husisha jamii hii ya Skull and Bones. -
Inasemekana kuwa Wakongwe Kama Prescott S. Bush ambaye ni baba wa Aliyekuwa Rais George W. Bush na Babu wa George W Bush huyu na wenzie wengine wanachama wa Skull and Bones walichimba mabaki ya Geronimo toka kaburini mwaka 1918 wakaiba fuvu la Huyu Shujaa, Na Mifupa miwili na mavazi yake kivita kutoka katika Kaburi lake huko Fort Sill. -
Jamii hii ikachukua mabaki haya na kuyaweka Makao yao Makuu ambayo yalikuwa yame anzishwa toka mwaka 1832.
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yaki zungumzwa kuhusiana na kundi au jamii hii. Inasemekana hawa ndio walio husika na utengenezaji wa bomu la nyuklia mpaka kuuawa kwa J.F. Kennedy Ingawa Pia Ina semekana Bwana Jf Kennedy alikua ana fahamu Juu ya hicho kifo chake. -
Ni kundi ambalo nchi za huku kwetu hali fahamiki na watu wengi lakini kwa Huko kwa wenzetu ni Kundi kubwa na la kutisha sana.
Ni Kundi lenye viongozi wakubwa sana duniani likihusishwa na miaka ile lilipokuwepo kundi la mafia kuwa hili ni kundi la mafia la kimataifa.
Pia Wana Patikana Katika Vyuo Vikuu Mbali Mbali Duniani na siku hizi hata Vyuo vya kawaida. -

Skull and Bones wamehusika na Kuendesha Utajiri wa Carnegie, Rockefeller na Familia ya Ford na pia kujihusisha na CIA, American Psychological Association, Baraza la Mahusiano ya Kimataifa na pia Baadhi ya Makampuni makubwa ya Sheria Kimataifa.
-
Mwaka 2004 wakati wa uchaguzi wa Urais wa Marekani walio kuwa wagombea wa Republic na Democratic walikuwa ni wanachama wa jamii hii. -
Johnn Kerry alipoulizwa jambo hili alijibu kifupi tu kuwa “Ni siri na siwezi zungumzia jambo hilo” na Bush W naye pia alipata kuzungumzia hili kwa hali ya kutotaka liendelee kuwa gumzo hivyo kwa Kiswahili kingine ni kuwa alilipotezea. Uhusika wa watu katika Jamii hii ni wa siri sana.
-
William Russell alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha YALE. Huyu ndiye aliyeanzisha jamii hii ya kishetani yenye nguvu kubwa bada ya kuwa aliwahi kukaa Ujeruman akiwa mwanchama wa kundi moja la siri sana duniani likiwepo kundi pia la ILLUMINATI. -
Rusell alirudi USA akiwa ame dhamiria kuanzisha jamii ya siri ya aina yake na akamwambia Alfonso Taft ambaye mtoto wake alikuja kuwa Rais William H Taft kuwa mmoja ya wanachama wa Kundi hili la Udugu wa Kifo “The Brotherhood of Death” ambalo baadaye ndo likaja kufahamiaka kuwa ni “The order of Skulls and Bones”, -
wanachama walikuwa waki muabudu Eulogia huyu ni mungu ambaye inasemekana alikuwa na nguvu za kufanya mtu awe na nguvu ya kuongea mbele za watu na kukubalika, kutukuzwa na kuwa mwenye Umiliki wa Dunia.
-
Fuvu na Mifupa ilianzishwa chuo kikuu cha yale ambacho ni cha Tatu kwa Uzaman Huko Marekani kwa maana ya kuwa ni chuo cha zamani sana katika namba ya vyuo vya zaman usa kinashika namba tatu.
-
Jamii hii imekuwa na ibada zake na mambo mablimbali ambayo yamekuwa ni alama zao pamoja na nyoka na kutoka sadaka zao kwa mungu wao.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages