》》mwandishi Imatheboy Classic
Joseph Kibwetere alikuwa ni kiongozi wa kidini (Mchungaji) wa kanisa la Vuguvugu la Urejesho wa amri kumi za Mungu (Movement of Restoration of Ten Commandments of God) lililokuwa likipatikana wilaya ya Kanungu - Magharibi mwa Uganda. Kundi hili lilitokana na waumini wa dini ya kikatoliki waliojitenga na taratibu za kikatoliki.
Joseph Kibwetere alizaliwa mwaka 1932, huko Kanungu. Mwaka 1960 Joseph Kibwetere alifunga ndoa na mwanamke ambaye baadae alikuja kumuacha. Mwanamke huyo alijulikana kwa jina la Tereza Kibwetere
Kibwetere alikuwa na watoto 16, kati yao 3 walikuwa wa nje ya Ndoa. Alitengana na mke wake mwaka 1992. Mpaka sasa mke wake huyo ambayw kwa saaa ni mzee sana anaishi eneo lijulikanalo kama Kabumba, wilaya ya Ntungamo.
Kitaaluma na kiweledi Kibwetere alikuwa ni mwalimu wa shule za msingi, na wakati flani aliwahi kuhudumu kama Msimamizi Msaidizi wa Shule katika Dayosisi ya Kikatoliki ya Mbarara.
Kibwetere amekulia katika familia ya kikatoliki, na ilikuwa ni familia iliyo bora kiuchumi kwa viwango vya Uganda wakati huo. Vilevile mbali ya kuwa mwalimu kitaaluma, Kibwetere alikuwa pia ni Mwanasiasa.
Mwaka 1980, Kibwetere alishiriki ktk siasa kugombea nafasi ya uwakilishi ya kisiasa nchini humo.
Kibwetere alikuwa na ardhi kubwa, na anakumbukwa kwa kutoa moja ya ardhi yake ili kuwezesha ujenzi wa shule, huku akitoa ushauri wa muundo wa shule hiyo kwa ukaribu sana. Shule hiyo iliitwa Ishaayuurirorya Maria Boarding
Mwaka 1984 Kibwetere akidai kuwa alikuwa akiuona upako wa Bikira Maria.
Mwaka 1989 alikutana na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Credonia Mwerinde. Huyu alikuwa ni mwanamke malaya aliyekuwa akijishughulisha na utengenezaji wa pombe ya asili maarufu kama 'Banana Beer' aliyekuwa akitafuta kutubu dhambi zake na kuanza maisha mapya. Maono ya Kibwetere kuuona upako wa bikira maria yalikolezwa na kupandikizwa kwake kisawasawa na mwanamama Credonia, ambaye na yeye alikiri kuwa na uwezo wa kumuona Bikira Maria.
Credonia alikuwa na historia ndefu katika masuala ya kudai kuona njozi na sura ya bikira maria. Alidai kwamba mara kadhaa alimuona Bikira Maria ktk miamba na milima. Credonia alitembea sehemu mbalimbali akiambataka na baba yake kuhubiri habari za Mungu waliyekuwa wakimuamini
Credonia alipokutana na Kibwetere alikaribishwa kwa mikono miwili na kusimuliana yale ambayo walidai Mungu aliwafungulia kuyaona na kuyatangaza Uganda nzima, hapo wakaanzisha kanisa la Movement for the Restoration of The Ten Commandments of God. Baba yake Credonia ndiye akawa Kiongozi mkuu wa kwanza wa kanisa hilo.
Baada ya baba yake Credonia kufariki, Kibwetere akarithi nafasi ya kuwa Kiongozi Mkuu wa kanisa hilo. Katika miaka ya 1990, kundi hili lilihubiri na kuhimiza sana kuhusu mwisho wa dunia. Credonia aliitoa ardhi ya baba yake ili itumike ktk kujenga makao makuu ya kubdi hilo la kidini. Credonia alijulikana kama Mpangaji au Mkuu wa mipangilio wa kanisa hilo 'Programmer' ila kiimani alijulikana kama 'Ishara ya Bikira Maria' (Ekyombeko Kya Maria) ikimaanisha Alama au Mfano wa Bikira Maria (Virgin Mary's Structure) Waumini waliamini kuwa Credonia ndiye aliyebeba baraka za Bikira Maria
》》IMANI YENYE UTATA WALIYOIAMINI BILA KUHOJI.
Machapisho na vitabu mbalimbali yaliyotolewa na kundi hilo yalihimiza kubusu dunia kufika mwisho na mambo mengine ya maisha baafa ya kifo. Mara kadhaa walitangaza kuhusu tarehe mbalimbali ambazo zingekuwa mwisho wa dunia lakini hakuna kitu kilichotokea. Tarehe zilizotangazwa zilipita bila chochote kutokea.
Mara kadhaa Kibwetere alinukuliwa akisema kuwa baada ya mwaka 2000 utafuatia mwaka mmoja wa dunia mpya. ( 1 year for new world)
Waumini waliaminishwa kuwa viongozi wao walikuwa wakiongea moja kwa moja na Mungu kupitia kwa Bikira Maria, pia waliaminishwa kuwa mwisho wa dunia umekaribia na kwamba ili usiende motoni au jehanamu yakupasa kuyafuata kwa ufasaha bila kukosea maelekezo ya dini hiyo yatokayo kwa viongozi wake (yaani akina Kibwetere)
Kundi hili lilianza kuhubiriwa habari ya mwisho wa dunia tangu mwaka 1992, wakati huo mhubiri wao wa kwanza aliitwa Martino Nuwagaba, ambaye aliwaaminisha kuwa Pasaka ya mwaka 1992 itakuwa mwisho wa dunia. Waliaminishwa kwamba siku za mwisho yatadondoka majoka makubwa kama tairi za trekta, na kwamba matofari ya zege yatadondoka duniani na kuwapiga wadhambi woote.
Walihubiriwa kuwa siku za mwisho wa dunia, giza litatanda dunia nzima na kwamba makanisa yao 'Camps' ndiyo itakayokuwa sehemu salama pekee ktk kuikwepa dhahama hiyo ya kiama, na kwamba makanisa yao ndiyo yatakayokuwa kama safina ya Nuhu.
Pia ilikuja kubainika kuwa, hata kile kitendo cha waumini hao kuziba madirisha na milango kwa misumari na mbao kabla ya kuwashwa MOTO ilikuwa ni ktk kuwahadaa waumini wao ili wajue kuwa giza lililotabiriwa ndilo hilo wanaloliona.
Waliaminishwa kuwa baada ya garika hiyo kushuka, watu woote duniani watakufa na kwamba waumini wa dhehebu hilo pekee ndiyo watakaosalia hai, na kwamba mali zote duniani, mashamba na nyumba za thamani zitakuwa mali yao. Maana wao pekee ndiyo watakaokuwa wamesalia duniani.
Kwa ufupi tu ni kwamba, katika kutimiza ibada yao, waumini na viongozi wa kundi hili walikiuka haki za msingi za binadamu mfano haki ya kuoa, kumiliki mali, huduma za afya, elimu nk. Hii ilitokana na mafundisho waliyopewa ambayo yaliwafanya waamini kuwa hawatakiwi kumiliki mali maana dunia inaelekea ukingoni, hawatakiwi kupata huduma za afya maana wanatakiwa kuombewa na kupona, hawatakiwi kuhangaika na elimu maana mwisho wa dunia umekaribia.
Katika kuhakikisha kuwa wanawazuia waumini/wafuasi wao kushirikiana na ulimwengu wa nje, walijenga kuta ndefu na nyeusi kuhakikisha kuwa hakuna aliyeweza kuona nje ya hapo, au wa nje kujua kinachoendelea ndani.
Hawakuruhusiwa kufanya mapenzi, yaani hata kama una mke au mchumba huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa.
Tofauti na viongozi wa kundi hili, wafuasi na waumini wengine hawakuruhusiwa kuzungumza kwa midomo. Bali walikuwa wakitakiwa kuongea kwa ishara pale wanapozungumza na wao kwa wao au wao na viongozi wao.
Mara nyingi viongozi wao waliwapangia ratiba iliyobanana kiasi kwamba walikosa hata muda wa kuzungumza na kujadiri masuala mbalimbali.
Walijisogeza ktk mifumo ya kiutawala, na wakawa wapole na wenye kutii taratibu zote za kiserikali. Hili liliwasaidia sana watu kutowatilia wasiwasi au mashaka yoyote. Kwa lugha rahisi ' Blending In'
Waliawaamuru wafuasi/waumini wao kuuza mali zao zote na kuwaletea fedha viongozi (Kibwetere) wao. Kwa kutumia mbinu hiyo walitengeneza jamii ya wafuasi wasiokuwa na kitu wala sababu ya kujitegemea, walitengeneza kundi la wafuasi ambao walibaki kuwa Manamba wa Fikra na tegemezi kwa kanisa ktk kila kitu.
》》KIAMA NA MAJONZI
Ulipofika mwezi wa tatu mwaka 2000 kundi hilo la Kibwetere likaanza kuchinja Ng'ombe na kununua soda nyingi aina ya Coca-Cola. Haya maandalizi hayakuwashtua watu, maana ilichukuliwa kama maandalizi kabla ya mfungo mkubwa uliotarajiwa kufuata.
Ilipofika tarehe 17 March 2000, ndiyo siku ambayo watu zaidi ya 530 walipokufa ktk kanisa la Kibwetere kwa kulishwa SUMU kisha KUCHOMWA moto mpaka majivu. Hata hivyo miili ya wafuasi wengine iliendelea kupatikana ktk Nyumba za waliokuwa viongozi wa kanisa hilo ikiwa imefukiwa ardhini baada ya kuuliwa siku kadhaa kabla ya siku yenyewe. Baada ya kujumlisha idadi yote ilikadiriwa kuwa zaidi ya watu 1000 walipoteza maisha ktk mauaji hayo ya haraiki. Baada ya tukio hilo, Familia ya Kibwetere ilidai kuwa Mwanamke Credonia ndiye aliyekuwa akimharibu (Bad Influence) Kibwetere na kumshawishi kujihusisha na matendo hayo maovu.
Mwaka mmoja baada ya mauaji hayo, kituo cha habari cha kimataifa cha BBC kiliripoti kuwa Kibwetere aliwahi kutibiwa ugonjwa wa 'Bipolar Disorder' huu ni ugonjwa ambao humfanya mgonjwa kuwa ktk vipindi vya msongo 'depression' msongo, hisia kali (elevated emotion) dhidi ya mambo mbalimbali na hata kufanya maamuzi ya kutaka kujiua, kulia hovyo, kukosa uaingizi, na hasira.
Baadae iligundulika kuwa waumini wa kundi la Kibwetere walitegemea unabii huo kutimia tarehe 31 Desemba 1999, na kwamba kilichotokea mwaka 2000 ni matokeo ya unabiii wa mwaka 1999 kushindwa kutimia. Waliamini dunia itafikia mwisho 31 Desemba 1999 lakini iliposhindikana ndipo hapo yakafuata maafa ya kupangwa.
Mwanzo iliaminika kuwa Kibwetere alikuwa miongoni mwa watu waliokufa kwa moto maana ikisadikiwa kuwa yale mauaji yalikuwa ni sehemu ya imani ya kanisa hilo kuamini kuwa wangeenda MBINGUNI kwa KUCHOMWA moto. Lakini Polisi nchini Uganda ilithibitisha kuwa tukio hilo lilikuwa limepangwa na kwamba Kibwetere na washirika wake waliwachoma watu hao kwa makusudi na kutorokea kusikojulikana
》》UNAJIFUNZA NINI??
Katika kuangazia maisha ya Kibwetere, Credonia Mwerinde, viongozi wengine wa kundi hili la kidini na waumini/wafuasi wao pamoja na imani waliyokuwa wakiifuata nimejifunza vitu kadhaa
i) Mwanamke ni mshawishi mkubwa sana katika maamuzi ya mwanaume. Credonia alifanikiwa kutawala na kumiliki akili ya Kibwetere.
ii) Popote pale unapoambiwa kufuata bila kuhoji lazima kuna shida mahala. Kuwazuia watu kujadiri na kuhoji ni Kuwapunguzia uwezo wa kutafakari maisha yao au hata maamuzi wanayopewa na viongozi wao.
iii) Kuna mambo ukiambiwa na kiongozi wako usiyafanye na ukakubali kutii bila kuhoji ni kipimo cha kiwangu kikubwa cha UJINGA ulio nao kichwani. Kumbuka waumini wa Kibwetere hawakuruhusiwa kuhoji, wala kuzungumza kwa sauti, kufanya mapenzi, kwenda hospitali wala kumiliki mali. Mpaka leo kuna viongozi wa siasa wanawaamrisha wafuasi wao au viongozi wenzao wasifanye mapenzi na mahasimu wao kiitikadi na wanatii bila kuhoji
iv) Hakuna mtu awaye yote, awe mchungaji au hata padre anayeweza KUMMILIKI Mungu. Hii tabia ya kuishi maisha ya kumuamini kiongozi wako wa dini zaidi hata ya unavyomuamini Mungu ni hatari sana ikiwa kiongozi huyo ataamua kufuata Nyayo za Kibwetere.
v) Akina Kibwetere bado wako wengi sana miongoni mwetu. Wako katika nyanja zote kuanzia makanisani, misikitini, katika vyama vya siasa, katika kampuni, serikalini, katika famikia zetu, waganga wa jadi nk nk nk
》》Karibu tena katika makala na biograph nyingine katika blog yako pendwa Imatheboy Classic
No comments:
Post a Comment