Historia ya Jehovah Wanyonyi Ambaye Alijiita mungu

Maisha ya Mzee Jehovah Wanyonyi ambaye katika uhai wake alijidai kuwa “mungu,’ yalikuwa fumbo  na sifa hizo zingali zinamwandama mautini hivi kwamba, wengi hawajui kwa uhakika kufikia sasa iwapo angali hai au aliaga dunia.

Lakini tathmini ya karibu ya maisha yake iliyofanywa na Taifa Leo imefichua mtu ambaye maisha yake yaligubikwa na usiri na wakati mwingine ulaghai wa aina fulani.
Mapema miaka ya ’60, aliishi na wafuasi wake katika kijiji kilichopo kilomita 30 kaskazini mwa mji wa Bungoma.

Waumini wake walitoa ardhi na mali nyingine kwa dhehebu lake kwa kuwa waliamini alikuwa na uwezo wa kuponya.
Waliokuwa fukara walijitolea kufanya kazi na kutoa mapato yao madogo kwa “mungu,” ambaye aliyagawanya miongoni mwao wote.
Walianza kutilia shaka nguvu zake kwani watu waliendelea kufariki kutokana na magonjwa tofauti.

Hali hii ilimfanya kuhamahama, ambapo alikita kambi kaskazini mwa Bondi la Ufa katika kijiji cha Kimalewa kilicho chini ya Mlima Elgon na Kaunti ya Uasin Gishu.
Alikuwa amedai mara tatu katika muda wa miaka 10 kuwa mwisho wa dunia ulikuwa umekaribia.

Thibitisho la kufariki kwake lililotolewa na serikali ni ishara nyingine kuwa alipotosha wafuasi wake.

Na sasa swali ni: 'Jehovah’ Wanyonyi” ni nani?
Wafuasi wake katika kijiji cha Chemororoch, eneobunge la Soy wangali bado wanasisitiza baba na mungu wao bado yu hai licha ya cheti cha kuruhusi mazishi yake kutolewa kwa wanahabari.

Wanyonyi anaaminika alizaliwa kati ya 1924 na 1925, Kaunti ya Bungoma, magharibi mwa Kenya.
Alikuwa na wake 70 na watoto zaidi ya 95
Katika mwaka wa 1956, alianzisha dini yake ambayo ilifahamika kama “Lost Israelites” (Waisraeli Waliopotea). Wenyeji waliita waumini wa dini hiyo “Baisraeli”.
Katika miaka ya ’60, alianza kuamini alikuwa na nguvu za kutenda miujiza ya kutibu magonjwa, akaamini hawezi kufariki na kujitangaza kuwa “Mungu wa kweli”.

Ishara zake za kidini zilikuwa pamoja na vazi lekundu, kitambara cha rangi nyeusi ama dhahabu, kilichofungwa kiunoni mwake na kofia nyekundu yenye nywele bandia zilizobandikwa kwa upande wa ndani.

Ilikuwa nadra sana kutoa kofia hiyo, lakini alipoitoa, kipara chake kiliweza kuonekana.
Mara nyingi aliambia wafuasi wake kuwa rangi nyekundu inamaanisha dunia itaisha karibuni na alikuwa akiketi kwa kiti chekundu na kubeba upanga ambao ala yake pia ilikuwa nyekundu.

Wakati wa sherehe za Krismasi, wafuasi wake walionyesha michezo ya kuigiza kuonyesha kusulubiwa kwake Kristo, kuimba nyimbo za kumsifu “mungu” wao na kualika umma kutazama mradi mtu asiulize maswali kuhusu uhalisia wa mungu wao.

Lakini pia alikuwa mhamaji. Kuanzia mapema miaka ya ’60, aliishi na wafuasi wake katika kijiji kilichopo kilomita 30 kaskazini mwa mji wa Bungoma.
Wafuasi wake walitoa ardhi na mali nyingine kwa dhehebu lake kwa kuwa waliamini alikuwa na uwezo wa kuponya.

Wale ambao hawakuwa na chochote, walijitolea kufanya kazi na kutoa mapato yao kwa “mungu”, ambaye kisha aliyagawanya miongoni mwa wafuasi wake. Lakini imani hiyo haikudumu.

Dhehebu kushamiri
Wakati baadhi ya wenyeji walipoanza kutilia shaka nguvu zake na kujiondoa, Wanyonyi alianza kuelekea kaskazini kwa kijiji kingine chini ya Mlima Elgon. Na hapo dhehebu lake lilianza kushamiri katika kijiji cha Kimalewa.
Katika kijiji hicho, alipata wafuasi waliokuwa tayari kujiunga naye kutoka kwa ukoo wa Bareefu wa kabila la Bukusu mojawapo ya makabila ya jamii ya Waluhya.
Mzee kutoka kwa ukoo huo, alitoa zaidi ya ekari 30 ambapo Mikaili na wafuasi wake walijenga nyumba zilizoezekwa kwa nyasi kabla ya baadaye kubadilika na kuwa zenye mabati.
Lakini wanakijiji waliishiwa na imani baada ya kubainika hakuweza kuponya watu maradhi aliyodai kuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Watoto zaidi walipokufa kutokana na malaria, watu kufa kwa kuugua homa ya matumbo na ueneaji wa HIV miongoni mwao, waliomkaribisha walichoka na kumtimua kutoka kwa ardhi yao.
Alikuwa amedai mara tatu katika muda wa miaka 10 kuwa mwisho wa dunia ulikuwa umekaribia.

Mnamo 2002, alitorokea Kaunti ya Uasin Gishu, ingawaje idadi ya wafuasi wake ilikuwa inadidimia. Wanyonyi alidai kuwa na “nguvu za kipekee” lakini alikuwa binadamu wa kawaida tu.
Alikuwa na wake 25, waliomzalia watoto 95. Baadhi ya wake zake walikuwa na umri wa hata miaka 16 alipotimiza umri wa miaka themanini, kumaanisha idadi ya watoto aliodai kuwa nao huenda si halisi.

Mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Muliro Telewa, ambaye alimhoji Wanyonyi 2001 eneo la Kimalewa, anakumbuka kumuona mwanamume akiwa katika umaskini na kuzingirwa na watu wenye njaa.
“mungu huyo” aliomba pesa za kuwalisha. “Hatukuwa na namna bali kutoa pesa zaidi kwa “mungu” ambaye watoto wake walikuwa na njaa ya kupata chakula cha kidunia,” aliripoti Telewa wakati huo.
Adhabu ya Ukimwi
Katika kisa kingine, Wanyonyi alitishia kuleta adhabu ya Ukimwi kwa Wakenya ikiwa serikali haingempatia Sh3 bilioni. Pesa hizo hazikuwahi kutolewa, lakini ueneaji wa Ukimwi bado haujabainishwa kwa laana yake.

Lakini je, alifaulu vipi kuwavuta watu wengi sana kuamini kuwa alikuwa mungu? Wanyonyi ingawaje hakujua kusoma na kuandika, alikuwa mwenye haiba kubwa.
Aliambia wafuasi wake kuwa alikuwa mungu aliyenena na watu kama ilivyoripotiwa katika Isaiah 11. Alifaulu kupanga dhehebu lake kuwa na uongozi dhabiti na mungu alikuwa juu.
Chini yake kulikuwa na mfalme wa amani ama mtume wa mungu, mwanamume mchanga aliyefahamika kama “Yesu” na ambaye kazi yake ilikuwa kuripoti shida za wafuasi wake kwake.
Kulikuwa na mapadri na manaibu wake ambao kazi zao zilijumuisha pia kuhakikisha kuwa “Jehovah” amelishwa ama walioamua ikiwa aongezwe mke.
Kisha kulikuwa na mhubiri mkuu, wanajeshi na wengine waliohusika na usalama.

Katika eneo la boma lake kulikuwa na jukwaa, ambapo mungu huyo pamoja na makanda wake waliketi.
Vile vile, kulikuwepo na “jela” lenye moto, ingawaje haijaweza kubainika ikiwa watu wowote wenye dhambi wamewahi kutumwa hapo kukutana na mwisho wao.
Kwa sasa imesalia kubainika ikiwa dhehebu lake litaendelea kudumu baada ya kuondoka kwake.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages