SOCIOPATH 3
Kwakuwa sociopath kiasili hujisikia raha kudhuru wengine, chunguza watu ulionao karibu je hujisikia raha kusingizia wengine, au hufanya matendo yasiyo ya kihuruma na hawa onyeshi kujutia, Una penda kumuona mtu yupo matatizoni?. Wana falsafa wanasema "when the deal is so good, think twice". Kuwa makini na watu wanao jifanya wema sana, kuna watu ni wema kiasili ni wema wame umbwa na roho hiyo na ni wengi sana. Kwakuwa Sociopath Wana hitajika kujificha, hujitengenezea mazingira ya kuto kutambulika na kuiaminisha jamii kuwa ni watu safi, kiasi kwamba hata ukija sikia wamefanya jambo fulani baya utashangaa.
Kwa tafiti zilizo fanywa na Shirika la REUTERS wengi wa wasanii, wanasiasa, waigizaji na viongozi wa asasi mbalimbali ina semekana ni Sociopath.
Mfano wa viongozi maarufu ni Mao Tse-tung ambaye ni baba wa taifa la CHINA anaye daiwa kubaka na kuua watu wengi kwa njaa.
Mwingine ni kiongozi wa zamani wa shirika la utangazaji la BBC anaitwa Jimmy Savile ,yeye alikuwa na genge la udharirishaji wa watoto. Aliendesha genge lake kwa miaka 40 bila watu kujua, mpaka alipo fariki.
Baadhi ya maswali ambayo watu wengi huuliza:
Je unajitambua kama wewe ni Sociopath?
Waweza jipima kama wewe ni sociopath au la? Je, unapata ugumu kuwaonea wengine huruma?
Je unapenda kuona wengine wanateseka au haujisikii lolote mtu mwingine anapoteseka? Je, kwa makusudi umewahi kutaka kumfanyia "kitu mbaya" mtu?
Je upendi kuona mwingine akifanikiwa?
Je, sociopath kuna kitu kinatokea unakuwa msababishi?
Sio lazima kitu kitokee wawe wame sababisha, kumbuka hawa sociopath hawana hisia zozote,
Je sociopath ni wazungu tuu kwa kuwa wazungu labda wanakuwa mara nyingi wanakua wapweke hawana cha kufanya kiasi kwamba Wana nyemelewa na hizo hisia?
Sociopath hajisikii kuwa mpweke. Hajui hizo hisia za kuwa mpweke, hajisikii kutaka kupendwa, hajisikii chochote.
Huyo ndio real sociopath. Hata hivyo Sio kila mtu mwenye kufanya jambo la ukatili ni sociopath. Kuna wanaofanya jambo baya wakajutia, pengine kwa hasira , au visasi, wakati mwingine mtu hufanya bila kukusudia ana jikuta tayari umesha tenda.
SOCIOPATH 3
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment