mlenga shabaha hodari wa Kikanada aliweka rekodi kwa kumtungua gaidi wa kikundi cha IS

Sniper au mlenga shabaha hodari wa Kikanada aliweka rekodi kwa kumtungua gaidi wa kikundi cha IS (Islamic State) “ daesh ”aliyekuwa umbali wa zaidi ya takribani maili 2. Katika kuweka rekodi hiyo, Sniper huyo alitumia silaha aina ya “ McMillan TAC-50 sniper rifle” akiwa juu ya moja ya majengo marefu inchini Iraq.
Risasi hiyo ilisafiri chini ya sekunde 10 kumi na kumuua gaidi huyo aliyekuwa umbali wa mita 3,540 (maili 2.19) mnamo mwaka 2017.
Tukio hilo lilivunja rekodi iliyowekwa mwanzo na mwanajeshi (sniper) wa Kiingereza Craig Harrison aliyewahi kumpiga adui (taliban) risasi akiwa kwenye umbali wa mita 2,475 (maili1.53) nchini Afghanistan (Helmand Province) mwaka 2009 akitumia “L115A3 long range rifle ”.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages