Huduma ya Kwanza kwa Mtu mwenye Mshtuko wa Moyo

Karibu katika blog ya Imatheboy Classic kipindi ni Afya
Leo tutauelezea Kuhusu Mshtuko wa moyo
Mshituko wa moyo unahitaji kushughulikiwa haraka. Kama unamshuhudia mtu akipatwa na mshituko wa moyo unapaswa kuomba msaada haraka au kumfikisha kituo cha afya haraka iwezekanavyo. Kama mtu aliyepatwa na
mshituko wa moyo amepoteza fahamu, baada ya kuomba msaada kituo cha afya cha karibu, unapaswa kumfanyia CPR mara moja kama unajua kufanya hivyo. CPR ni kitendo ambacho husaidia kufikisha hewa ya oksijeni katika
ubongo. Kwanza hakikisha njia za hewa za mgonjwa ziko wazi, yaani hakikisha mdomoni na puani kwake hakuna kitu kinachozuia hewa kupita na msaidie kwa hewa kila baada ya kumkandamiza kifuani au (chest compress)
mara 30. Kama hujuia CPR pia unapaswa kuanza kumkandamiza kifuani mgonjwa aliyepoteza fahamu kutokana na mshituko wa moyo, kwani kufanya hivyo huenda kukaokoa maisha yake. Tutaelekeza hapa jinsi ya
kumkandamiza kifuani mgonjwa aliyepatwa na mshituko wa moyo na aliyepoteza fahamu. Weka kiganya cha mkono wako mmoja katika mfupa wa kifua (chestbone) katikati ya matiti na kiganya cha pili juu ya cha kwanza, na
kandamiza kwa kiasi cha inchi mbili au sentimeta 5 kuelekea chini. Eendelea kukandamiza na kuachia mara 30. Kama unajua namna ya kufanya CPR mfanyie mgonjwa na kama hujui endele kumkandamiza sehemu hiyo ya kifua hadi msaada utakapowasili au hadi mgonjwa atakapopata fahamu au kuonyesha dalili za kupumua.
MATIBABU.
Matibabu ya ugonjwa wa mshituko wa moyo hufanyika hospitali kwa njia tofauti kulingana na hali ya mgonjwa. Kila dakika inavyopita baada ya kutokea mshituko wa moyo, ndivyo tishu ya moyo inavyopoteza oksijeni na kuharibika au kufa. Njia kuu ya kuzuia moyo usiharibike ni kurejesha tena haraka mzunguko wa damu. Mgonjwa wa mshituko
wa moyo huweza kutibiwa kwa dawa au njia nyinginezo za tiba kwa kutegemea jinsi gani tishu ya moyo ilivyoharibika. Dawa tofauti zinazotumika kutibu mshituko wa moyo ni kama aspirin, dawa zinazoyeyusha damu ili
kuondoa damu iliyoganda ambazo huitwa kitaalamu kama clot buster, dawa aina ya heparin na nyinginezo ambazo hutofautiana kutokana na utendaji wake mwilini. Baadhi ya wakati athari za mshituko wa moyo huwa kubwa ambapo mgonjwa hutibiwa kwa njia inayoitwa Angioplasty. Hiyo siyo operesheni bali ni matibabu ya
kufungua mishipa ya damu iliyoziba au kudhoofika na kusabisha mshituko wa moyo. Mara nyingine wagonjwa wa heart attack hutibiwa kwa upasuaji unaoitwa bypass surgery.
Baada ya kujua namna ya kutibu mshituko wa moyo, sasa tuangalie ni jinsi gani tunaweza kujiepusha na ugonjwa huo wenye madhara makubwa kwa miili yetu.
Kwa wale ambao tayari wameshapatwa na ugonjwa huu pia wanashauriwa kuendelea kutumia dawa walizopewa hospitalini lakini pia kubadilisha mienendo ya maisha yao ili kuzuia kupatwa tena na mshituko wa moyo katika siku
zijazo. Kwa wale ambao mshituko wao wa moyo umesababishwa na magonjwa mengineyo waliyonayo kama matatizo mengine katika moyo au maradhi tofauti, wanatakiwa kutibiwa maradhi hayo. Lakini kwa ujumla tunaweza
kujiepusha kupatwa na ugonjwa huo kwa kutovuta sigara, kudhibiti hali nyinginezo kama shinikizo la damu, ongezeko la mafuta ya kolestroli mwilini na kisukari. Suala jingine linaloweza kuzuia kupatwa na shinikizo la damu
ni kuushughulisha mwili kila mara na kufanya mazoezi, kupata lishe bora, kupunguza uzito uliopindukia wa mwili na kupunguza ua kujiepusha na wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo.
Kama ndio kwanza unafungulia redio yako mpenzi msikilizaji kilichopo hewani ni kipindi cha Ijue Afya Yako kinachowajia kupitia Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mada tunayozungumzia ni mshituko wa moyo. Kama wewe ni mvutaji wa sigara, tafadhali acha kuvuta sigara ili ujiepushe kupatwa na heart
attack na kama unaishi katika mazingira ambayo kuna mtu au watu wanaovuta sigara, basi washauri wenzako waache kuvuta sigara kwani sio tu tabia hiyo huathiri afya zao bali yako wewe pia. Vile vile matumizi ya tumbaku
yana taathira kama ya sigara kwenye moyo. Tunashauriwa kufanya mazoezi kwa uchache dakika 30 kwa wiki ili kujiepusha na ugonjwa wa moyo. Mazoezi hayo yanaweza kuwa ya aina yoyote hata kutembea kwa mguu. Hii ni katika hali ambayo, lishe ina nafasi muhimu katika kuwaepusha watu kuwa na unene wa kupindukia na hivyo kutokupata mshituko wa moyo.
Dakta Linda Van Horn mtaalamu wa lishe na mjumbe wa Kamati ya Lishe ya Jumuiya ya Moyo ya Marekani ambaye pia ni mhadhiri wa tiba ya kuzuia maradhi katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Northwestern huko Chicago anashauri kuwa, ili kujikinga na mshituko wa moyo tunapaswa kula vyakula vyenye ufumwele kwa wingi na
visivyokuwa na mafuta mengi ili kuimarisha afya ya mioyo yetu. Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yasiyo na madhara au unsaturated fats kama vile fati asidi za omega 3 na mafuta ya zaituni huweza kusaidia kupunguza
kiwango cha mafuta yenye madhara katika miili yetu, kuzuia damu kuganda na pia kufanya chembe za mafuta zisigande katika mishipa ya damu. Lishe iliyo na ufumwele ambayo mara nyingi hupatikana katika nafaka, baadhi
ya matunda na mboga, husaidia kupunguza kolestroli aina ya LDL ambayo ni hatari kwa miili yetu. Baadhi ya vyakula vyenye uwezo wa kuimarisha afya ya mioyo yetu ni samaki hasa aina ya sardine na salmon. Samaki hao wana kiwango kikubwa cha omega 3 pamoja na calcium na niacin ambazo ni virutubisho muhimu kwa afya zetu. Chakula kingine ni shayiri yenye ufumwele kwa wingi na pia huupatia mwili nguvu kwa haraka na kuzuia njaa kwa muda mrefu.
Wasikilizaji wapenzi utafiti umeonyesha kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku kunapunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo. Utafiti huo uliotolewa katika Kongamano la Jumuiya ya Mshituko wa Moyo
la Kimataifa nchini Marekani, umeeleza kwamba kunywa kikombe kimoja cha kahawa ya kawaida na isiyokuwa na kafeini kila siku huzuia kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 30. Hata hivyo wataalamu wameonya kuwa
kutumia sana kinywaji hicho matokeo yake yanaweza kuwa kinyume. Utafiti mwingine umeonosha kuwa, kufanya mazoezi kwa muda mrefu hakuhusiana na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Huko nyuma kulikuwepo
tafiti zilizoonesha wasiwasi wa afya ya mishipa ya moyo kwa baadhi ya wanamichezo wa Olimpiki. Tafiti hizo zilisema kwamba, kupanuka kwa mioyo ya wanamichezo kunakoitwa kitaalamu "athlete's heart" huufanya moyo kuwa dhaifu sana na kushindwa kuvumilia mazoezi mazito. Lakini kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa kwenye
jarida la Marekani la Kitengo cha Magonjwa ya Moyo, mazoezi mazito hayana hatari kwa afya ya moyo. Kiwango cha damu inayosukumwa katika miili ya wanamichezo hakibadiliki wakati wa mazoezi. Mbali na kupanuka kidogo baadhi ya sehemu za moyo, misuli ya moyo hubakia sawa wakati wa mazoezi. Wanasayansi wamehitimisha
kwamba, mioyo ya wanamichezo ina afya nzuri na inaweza kuvumilia kirahisi mazoezi ya kiwango cha juu. Pia wamesema kwamba, baadhi ya dawa kama vile erythropoietin (EPO) zinazotumiwa na wanamichezo hao ili kuzipa nguvu chembe chembe nyekundu za damu, kunaufanya utendaji kazi wa moyo udhoofu, suala ambalo limekuwa likiwaathiri wanamichezo hao na wala sio mazoezi mazito ya mwili wanayoyafanya.
Naam wapenzi wasikilizaji, kabla hatujahitimisha kipindi chetu sio vibaya ukijua kuwa, moyo ulioko katika kifua cha mwanadamu hupiga mara 100,000 kwa siku, husukuma galoni mbili za damu kwa dakika, galoni 120 kwa saa na
hufanya hivyo kwa masaa 24 kwa siku, miezi na miaka yote mwanadamu anayoishi duniani. Mfumo wa mishipa ya damu ambayo
husafirisha damu katika mwili wa binadamu ina urefu wa maili 60,000. Ukubwa huo ni mara mbili zaidi ya mzunguko wa dunia!
Suala la kustaajabisha zaidi na unalopaswa kujua kuhusiana na kiungo hiki muhimu katika mwili wa binadamu ni kwamba moyo huanza kupiga katika mwili wa mtoto mchanga pale anapoumbwa tumboni, hata kabla ubongo haujaumbwa. Moyo huanza kupiga kabla hata ya mfumo wa fahamu wa kati kuumbwa! Kuna nadharia maarufu
kwamba mfumo wa kati wa fahamu (CNS) hudhibiti na kusimamia vitendo vyote vya mwanadamu kuanzia kwenye ubongo lakini utafiti umeonesha kwamba mfumo wa fahamu hauanzishi mapigo ya moyo. Kiuhakika mapigo ya
moyo huanza yenyewe na kuna wanaosema kuwa bado haijafahamika mapigo ya moyo huanzishwa na nini. Wataalamu wanasema kuwa moyo ni kituo cha ufahamu (consciousness) na wala sio ubongo kama wengi tunavyodhani. Daima tuzilinde afya zetu!

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages