Skimmers
Hii ni mbinu ambapo mwalifu anahitaji kutumia Kadi feki ya ATM (Clonned cards) maalumu ilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana ambayo ina uwezo wa kuiba taarifa za kibenki za wateja na kumwezesha mwalifu kupakua pesa kutoka kwenye account mbali mbali kutumia mashine ya ATM. Kadi hizi zimeikuwa clonned na programu ya MRS606 pamoja na malicious softwares zingine za wizi wa mtandaoni.
Kwa maelezo ya Hacker maarufu. ni kwamba alinunua kadi hii Wall street, NY kwa gharama ya dola za kimarekani 170,000. Anachokifanya yeye ni kupambana kupata namba ya akaunti yoyote ile (Kama ulishawahi kukutana na zile scam za FB mtu akijitambulisha kua ana pesa nyingi, umtumie namba yako ya akaunti akurushie pesa), huwa wanatumia mbinu nyingi sana pamoja kupita kwenye dust bins za mabenki na mashine za ATM kuchukua risiti zenye namba.
Baada ya hapo ataichukua card hiyo na kuingiza kwenye mashine maalumu ambayo anaiunganisha kwenye computer, hiyo card itasoma kama 'free card' ataingiza ile account namba aliyoipata. Muda tu ambao yule mteja mwenye akaunti orijino atatumia ATM card yake basi Software maalumu iliyopo ndani ya card fake ya Hacker computer na mashine itaweza kutoa taarifa zote za kibenki ikiwemo salio likilopo pamoja na 'password' ya account number iliyoingizwa. Baada ya hapo bila wasiwasi wowote Hacker ataenda ATM kuchomoa pesa kwa furaha tele na kuendeleza maisha ya Teknologia yake.
Hackers Wanaotumia njia ya Skimmers kuiba kwenye mabenki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment