BOMU LA NYUKLIA - 2

BOMU LA NYUKLIA - 2
》Kihistoria mji wa Hiroshima ambao uliathiriwa na bomu la nyuklia ni mji Mkuu wa Mkoa wa Hiroshima Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2009, mji una wakazi wapatao milioni 1.2 wanaoishi katika mji huu. Mji huu uko kwenye kisiwa kinachojulikana kama Honshu. Mji umekuwa maarufu duniani kwa sababu ilikuwa mji wa kwanza katika historia iliyoshambuliwa kwa bomu ya nyuklia. Mji huu ulijengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Katika mji huu kuna gofu ambalo linajulikana kama ‘Kuba ya Bomu ya nyuklia’ ni gofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko, na jengo hilo limeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia. Kabla tya kushambuliwa mji huu ulikuwa na msongamano wa watu waliokuwa wakifikia 381,000 lakini baada ya vita kuisha idadi hiyo imepungua na kufikia kiasi cha watu 255,000. Mji mwingine ulikumbwa na shambulio la mabomu hayo ulikuwa Nagasaki ambao nao unapatikana katika kisiwa cha Kyushu. Mji huu nao umejizolea umaarufu kutokana na shambulio hilo la mwaka 1945 na kwa sasa unatumiwa kama mji wa pili wa kihistoria baada ya Hiroshima. Mji huu ulipopigwa na bomu ulisababisha mauaji ya watu 36,000 hapo hapo na wengine waliokadiriwa kuwa kati ya 70,000 na 100,000 kufariki baadaye kutokana na maradhi yaliyotokana na nyuklia. Kabla ya angamizi hilo Nagasaki ilikuwa kitovu cha Ukristo katika Japani mnamo mwaka 1600 na imani hii ya Kikristo ilipigwa marufuku na serikali ya Japan. Agizo hilo la kupigwa marufuku kwa Ukristo ilisababisha wakristo wengi kuuawa katika miaka iliyofuata na wapo walitunza imani hiyo kwa siri hadi kurudishwa kwa uhuru wa kuabudu katika karne ya 19. Kanisa lililokuwa maarufu la Kikatoriki huko Nagasaki linalojulikana kama, Urakami Tenshudo liliharibiwa na bomu la nyuklia Januari 1946. Pia katika mauwaji hayo inadaiwa asilimia 90 ya madaktari waliuawa ikiwa ni pamoja na asilimia 93 ya wauguzi wa Hiroshima. .
Itaendelea....

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages