BOMU LA NYUKLIA - 1 .
》》Bomu la nyuklia ni silaha inayosababisa mlipuko mkubwa sana na ni silaha hatari na yenye nguvu kuliko silaha yoyote iliyowahi kupatwa kutengenezwa katika historia ya silaha Duniani. Mabomu haya ya atomi hutengenezwa kwa kutumia madini yaitwayo Uraniamu au Plutoni. Pindi lipigwapo bomu hilo husababisha kuondoa kila inachokikuta katika uso wa dunia na kugeuza eneo hilo na kuwa jangwa. Teknolojia ya kufyatua mabomu ya nyuklia Kuna hasa namna mbili za kufikisha mabomu haya panapolengwa njia ya kwanza ni kutumia ndege za kivita na njia ya pili ni kutumia roketi. Pia kuna mabomu madogo yanayoingizwa katika makombora ya mizinga. Nchi ya Japani kila Agosti 6, haitaweza kusahau tukio la kupigwa bomu la Nyuklia katika miji yake ya Hiroshima na Nagasaki ikiwa katika vita ya pili ya dunia ikielekea kufika ukomo. Japani ilijikuta ikipata kipigo hicho kitakatifu kutoka kwa Marekani ambayo iliamriwa kufanya hivyo na rais wake Harry S. Truman, kupiga mabomu hayo mfululizo kutokea Agosti 6 hadi Agosti 9, 1945. Bomu hilo ambalo lilipewa jina la ‘Little Boy’ liliporomosha jiji la Hiroshima siku ya jumatatu, Agosti 6, 1945, hadi Agosti 9 likamaliziwa na Nagasaki na kuandika historia ambayo haitasahaulika duniani. Mlipuko huo hasa ndiyo uliosababisha kupinga utengenezaji wa mabomu ya aina hiyo kwani ulifanya maangamizi makubwa kwa kuua jumla ya watu 140,000 huko Hiroshima na 80,000 wa Nagasaki mwishoni mwa mwaka 1945. Siku chache baada ya kumalizika kwa tukio hilo inakisiwa kuna asilimia kati ya 15 na 20 ya watu waliopoteza maisha kutokana na majeruha waliyoyapata kutokana bomu hilo. Wapo waliofariki kutokana na hewa ambayo ilikuwa ya sumu kutoka katika bomu hilo, wengine walikufa kutokana na mionzi yake na wengine kansa. Kutokana na uwezo wa mabomu hayo siku sita ya kupigwa kwake huko Nagasaki, Agosti 15, Japani ilitangaza Kusalimu amri na Septemba 2 ilisaini kuachana na vita hivyo. Mradi huu ulipewa jina la ‘The Manhattan Project’ ulikuwa wa kwanza kutengenezwa ukiwa chini ya ushirikiano kati ya wataalamu kutoka Marekani, Uingereza na Canada.
Itaendelea......
BOMU LA NYUKLIA - 1 .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment