Usimpe asali mwanao mchanga!
Pengine umewahi kumlambisha asali mwanao mchanga (mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja). Umempa ili kulainisha koo hasa mtoto anapokuwa na kikohozi.
Ni hatari kumpa mtoto mchanga asali. Asali hasa asali mbichi inaweza mbegu za bakteria waitwao Clostridium botulinum. Bakteria hawa wanapoliwa huzalisha sumu kali mwilini na kusababisha ugonjwa uitwao Infant botulism.
Ugonjwa huu ni hatari sana. Mtoto akipata ugonjwa huu yupo katika hatari kubwa sana ya kupoteza maisha.
Zingatia: Epuka kumpa mtoto mchanga asali hata kama ni tone au kwenye chakula. Unaweza kumpa asali mtoto ambaye ana zaidi ya mwaka mmoja.
Share habari hii na wazazi wote ili wawe makini
Like hii page ili usipitwe na elimu kama hii
Swali au maoni..uliza kwenye comments hapo chini! au Piga 0715116975
Asali Haifai Kwa Watoto wachanga chini ya Mwaka Mmoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment