Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani likitanguliwa na Asia. Lina ukubwa wa takriban kilometa za mraba milioni 30.3.
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2016 Afrika ina jumla ya watu 1.2 Billion ikiwa sawa na 16% ya idadi ya watu waliopo duniani kote.
Mambo haya 10 kama Afrika tunajivunia nayo
1. Equatorial Guinea ni nchi Pekee Afrika ambayo lugha yake ya Taifa ni Kihispaniola (Spanish). Hakuna nchi nyingine inayozungumza kihispaniola.
2. Nchi ya Gambia ina chuo kikuu kimoja tu (The University of Gambia)
3. Nigeria imeshinda vikombe vingi vya soka kuliko England
4. Angola ina watu wengi wanaoongea kireno kuliko Ureno yenyewe. Angola ina watu million 22 na wote wanaongea Kireno lakini Ureno ina watu million 10.7 pekee
5. Raia kutoka Nigeria anaitwa Nigerian, kutoka Niger anaitwa Nigerien kutoka Burkina Faso anaitwa Burkinabe
6. Nigeria ndio nchi yenye matajiri wengi weusi kuliko nchi nyingine Afrika
7. Afrika Kusini ndio nchi inayotembelewa sana kuliko nchi yoyote Afrika
8. Mauritius ndio nchi inayoingiza fedha nyingi zaidi kwa kutumia vivutio vya Utalii walivyo navyo.
9. Somalia ilipata mashine ya kwanza ya ATM mwaka 2014
10. Zanzibar ni nchi ya kwanza Afrika kumiliki televisheni ya Rangi .
Mambo ya Kujivunia Afrika Yetu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment