Kisiwa Kwa Ajili ya Wanawake Nchini Ufilipino!

Nchi ya Ufilipino (Philippines) ni moja ya taifa linalothamini harakati za wanawake kwa kiwango kikubwa.
Kutokana na tamadauni zao mwanamke anahesabika kama mtu jasiri, mwenye uwezo wa kufanya kila jambo.
Agenda kuu duniani kote kwa sasa ni usawa wa kijinsia lakini hasa kwenye mataifa yanayoendelea lengo likiwa ni kuwapa wanawake haki zao za msingi ili waweze kufurahia maisha ya kila siku.
Nchini Ufilipino wao wamepiga hatua kwenye hili kwani kwa sasa wanajenga kisiwa ambacho ni maalum kwa wanawake tu ambapo watatumia kisiwa hicho kwa ajili ya kupumzika na kufurahi.
Kisiwa hicho kiitwacho SuperShe kinamilikiwa na binti anaejulikana kwa jina la Christina Roth amabe ni mjasiriamali na na mwanzilish iwa blogu ya mitindo iitwayo SuperShe .
Kisiwa hiki kikianza kutumika kitamuhitaji mwanamke anaetaka kwenda kutembea alipe Dola za kimarekani 3,500 (Milioni 8.5 za kitanzania) kwa kipindi cha wiki moja na kisiwa hiki kitazinduliwa mwaka huu 2018 ingawa haijajulikana tarehe rasmi .

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages