Fuatana nami ili uweze kupiga windows 7 katika mashine yako bila malipo yeyote
1:Ingiza CD yako katika DVD-ROOM ya mashine yako kisha subiri CD yako isome ikisha soma Restart mashine yako kisha bonyeza Boot Button, hapa kila mashine huwa zinatofautiana ila nyingi ni F8, F10 au F12, so angalia mashine yako boot button yake ni ipi.
Kama itagoma usichoke rudia tena ila ikikubali
2:Fanya machaguo sahihi hapo katika Lugha, Time na type ya keyboard sasa bonyeza Install Now
Weka tiki katika kibox ili kukubaliana na sheria za microsoft kisha bonyeza next ili kuendelea
3:Bonyeza Upgrade kama ulikuwa na Windows 7 na unataka kuibadilisha...Au bonyeza Custom (advanced) huna Windows 7 na unaweka windows 7 upya
Chagua Drive kama ni (C:) AU (D:) ambayo unataka kuweka windows 7
4:Bonyeza Drive options (advanced) kama unataka kutengeneza Partiton (Kuigawanya hard disk ) Kisha bonyeza Next, sasa windows yako itaanza mchakato wake wa kujiweka katika mashine yako
5:Baada ya michakato hiyo mashine yako itajizima na kujiwasha usiogope bado ipo katika mchakato
Ikishajiwasha itaendelea na mchakato wa setup iliyobakia itachukua muda kidogo wenda ikazidi ule muda wa mwanzo lakini usijali itamaliza kisha itajizima na kujiwasha kwa mara ya pili.
6:ikishawaka sasa itakupa chaguo la kuandika jina unaweza kuandika jina lolote ulipendalo pia ukipenda unaweza kuweka na Password lakini kama hautopenda andika jina tu kisha bonyeza next, wenda ikakuomba Keys chukua hapa kama hauna lakini pia unaweza kubonyeza next bila kuweka ila itakuja kukuomba baadae
Bonyeza next kisha set vitu hivi chini pichani kama utakavyopenda wewe
7;Mpaka kufikia hapo tayari mashine yako kwa kutumika Imeandikwa na Imatheboy Classic Picha kutoka Mtandaoni. kama hujaelewa au unaswali lolote kuhusu mada hii niachie maoni yako hapo chini.
No comments:
Post a Comment