Huduma ya kwanza

Huduma ya kwanza inamaanisha
huduma au msaada unatolewa kwa
mtu anayekabiliwa na ugonjwa au ma dhara ya ghafla wakati daktari hayupo karibu na kabla hajapelekwa
hospitalini kwa matibabu zaidi.
Kwa mfano huduma ya kwanza inatolewa wakati mtu anapopatikana baada ya ajali amejeruhiwa kwa
shabaha ya kutunza uhai wake hadi
mganga atakapopatikana au mjeruhiwa atakapoweza kufikishwa
hospitalini .
Shabaha nyingine ni kuzuia kuongezeka kwa madhara kwa mfano kwa kumwondoa sehemu yenye hatari kama moto, hatari ya mlipuko au mahali penye hatari kwake binafsi.
Huduma ya kwanza inaweza pia kutaja misaada midogo kama kumpatia mtu
plasta ya kufunika kidonda kisicho kikubwa.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages