Presha ya kushuka(Low Blood Pressure) au kwa kitaalamu huitwa Hypertension, hali hii hutokea pale msukumo wa damu unapokuwa mdogo na dhaifu. Hali hio husababishwa na viungo vya mwili mfano ini, mapafu, moyo kushindwa kupokea kiasi kinachojitosheleza cha damu na hewa ya oxygen.
Ugonjwa huu unasababishwa na mshtuko, kukata tamaa, mawazo yaliyopitiliza, ukosefu wa maji mwilini na wakati meingine mwili kukosa vitamin, madini na protini ya kutosha.
Mwenye shinikizo la damu la ain hii anaweza kuona tofauti kwenye mwili wake na kujisikia mdhaifu ghafla, macho kupoteza nguvu ya kuona, midomo kukauka, kizunguzungu na hatimaye kuanguka na kupoteza fahamu.
Ukiona mtu mwenye dalili hizo ni vyema ukamsaidia kwa kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.
Namna ya kufanya
Kama mtu ataanza kusiki akizunguzungu, mkalishe katika kiti au umlaze chini na unyanyue kichwa chake na kuweka mto chini yake. Unaweza kumnywesha maji uliyochanganya na chumvi.
Kuwa makini unapomuinua kutoka chini au sehemu aliyokuwa amekaa. Muinuko wa ghafla unaweza kuzidi kupunguza msukumo wa damu.
Hali hii ikiendelea hivyo kwa muda, mfunge mgonjwa katika mguu wake umbali wa nchi kama tano hivi chini ya goti kwa kutumia lastiki au mpira unaovutika ili kuzuia damu isiende chini ya miguu kusudi ibakie hasa sehemu ya juu ya mwili.
Maziwa ya mtindi yanatajwa kuwa dawa inayosaidia kwa mgonjwa wa shinikizo la damu la kushuka.
Kwa uhakika wa matibabu, tafuta usafiri kisha mpeleke mgonjwa wako hospitali au zahanati au kituo cha afya kilicho karibu kwa ajili ya kupatiwa huduma zaidi.
HUDUMA YA KWANZA KWA MTU MWENYE PRESHA YA KUSHUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment