Msaidie muathirika kutoka kwenye Maji . Ingia kwenye maji kumuokoa kama ni mtoto aliyezama au wewe ni mtaalamu wa kuokoa watu majini (lifeguard),kama wewe ni Mtu wa kawaida haushauriwi kuelekea katika kina kirefu cha maji kwaajili ya kumuokoa mtu huyu. Kwani mtu anapozama majini huwa na nguvu sana kiasi cha kuweza kukujeruhi na kukuzamisha nawe pia. Cha kufanya; chukua kamba ndefu au fimbo na umrushie ili aishike, na kisha umvute kutoka kina kirefu na kumweka nchi kavu. Unaweza kufungia kitu mwishoni mwa kamba ili muathirika aweza kuikamata kamba vizuri.
》》Huduma ya kwanza.
Baada ya kumtoa muathirika majini unaweza kufanya yafuatayo.
1. Kama hajapoteza fahamu na anakohoa, mhamasishe akohoe ili kusaidia kutoa maji kwenye njia ya hewa na mapafu.
2. kama amepoteza fahamu au hajiwezi. Chunguza kama anaweza kupumua kama ifuatavyo; weka sikio lako mdomoni kwake na usikie kama hewa unatoka, pia tazama kama kifua kinapanda na kushuka. Pia tazama kama ana majeraha yoyote dhahiri.
3. Kama anapumua mlaze kwa ubavu kama ilivyoonyeshwa katika picha hapa chini, huku ukihakikisha kwamba mdomo wake unabaki wazi ili kuruhusu maji yatoke.
《Angalia pichani Namna ya kumuweka mtu aliyezama majini kuruhusu maji yatoke kinywani》
4. Kama hawezi kupumua, mlaze chali na ‘ikiwezekana’ mpe pumzi za mdomo kwa mdomo (mouth to mouth breathing) kwa kubana pua yake na kumpulizia kwa nguvu(kama ni mtu mzima) au taratibu kwa mtoto. Mpe pumzi hizi mara nne kisha tazama tena kama anapumua.
5. Waweza kurudia hatua ya 3 na 4 hadi muathirika atakapoweza kupumua au msaada zaidi utakapopatikana.
6. Ni muhimu sana kumpeleka muathirika hospitali hata kama akipata nafuu, kwaajili ya matibabu zaidi maana anaweza kupata athari za muda mrefu kama pneumonia, matatizo ya moyo, na pia anaweza kuwa amepata majeraha yasiyoonekana kirahisi.
》》Muhimu : Kuna haja ya msingi sana ya muokoaji kujikinga na magonjwa mengine ambukizi kama VVU (HIV), virusi ya Homa ya manjano (hepatitis B virus) na mengineyo hasa wakati wa kumpa mgonjwa pumzi. Hivyo usimpe pumzi mtu usiyemfahamu au kujua afya yake bila kutumia vifaa maalumu vya kujikinga.
No comments:
Post a Comment