1. Zinedine Zidane aliwahi kurudi nchi yake ya asili Algeria ili aichezee kwenye mashindano ya kimataifa. Alipofika waziri wa michezo wa Algeria, Abdelmalek Sellal akamwambia "tuna wachezaji wengi wazuri kuliko wewe na hawajapata nafasi kwenye kikosi. Labda tungeruhusiwa kucheza zaidi ya 11 uwanjani ungeweza kubatika kupata namba"
2. Robert Mugabe ndiye Rais mzee zaidi duniani. Anashikilia rekodi kwa kuwa na umri wa miaka 91 akifuatiw na Shimon Peres, Rais wa Israeli mwenye miaka 90.
3. Shelisheli (Seychellois) ndio nchi y kwanza duniani ambayo raia wake wameelimika kuliko nchi nyingine. Inakadiriwa kuwa asilimia 91.9% ya watu wake wana elimu ya sekondari na kuendelea. (Tanzania wenye elimu ya sekondari na kuendelea ni asilimia 13.5 kwa mujibu wa HakiElimu.)
4. Mauritius ndiyo nchi pekee Afrika inayoingiza fedha nyingi kupitia utali wa fukwe (Beach Tourism). Mwaka 2013 iliingiza takribali shilingi trilioni 4.5 kupitia utalii wa fukwe. Tanzania tuliingiza shilingi bilioni 1.7 kupitia Utalii wa fukwe mwaka huohuo.
5. Rwanda ndiyo nchi pekee yenye usawa wa kijinsia kuliko nchi zote duniani (Bunge la Rwanda ni 50% wanaume na 50% wanawake).
6. Ethiopia ndio nchi pekee Afrika yenye viwanja vingi vya ndege vyeny hadhi ya kimataifa (International Airports). Ina viwanja vya ndege 23 vyenye hadhi ya kimataifa. (Tanzania tuna viwanja vya ndege vitatu vyenye hadhi ya kimataifa (JNIA-Dar, KIA-Moshi, na Songwe-Mbeya).
7. Uchumi wa Ethiopia unakua kwa kasi kuliko Uchumi wa China. Uchumi wa Ethiopia (GDP) unakua kwa wastani wa 18.7% kwa mwaka, China GDP inakua kwa wastani wa 11.4% kwa mwaka (according to the World bank fact sheet, 2014)
8. Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ndiye Rais Maskini kuliko wote Afrika Analipwa mshahara wa Dola 500 za kimarekani ($ 500) sawa na Shilingi 945,000/=. Hiki ni kiwango kidogo cha mshahara kuliko daktari wa mfunzo nchini Tanzania (Intern Doctor).
9. Angola ina watu wengi wanaoongea Kireno kuliko Ureno kwenyewe. Angola ina watu milioni 2 na wote wanaongea Kireno, lakini Ureno ambao ndio wenye lugha wana watu milioni 10.7 tu.
10. Somalia ilipata mashine yake ya kwanza ya ATM tarehe 7, October, 2014. Kabla ya hapo hakukuwa na ATM yoyote nchini Somalia.
Fahamu zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment