Adolf Hitler alikuwa na Korodani moja Tu

Inasemekana kuwa Dikteta wa zamani kutoka Ujerumani, Adolf Hitler alikuwa na Korodani moja tu .
Kipindi cha Vita ya pili ya Dunia unaambiwa Waingereza walikuwa na Wimbo, wakimtusi Hitler kwa kuwa na korodani moja, Wimbo ambao hadi leo unaambiwa watoto huwa wanaimba.
Kwa kipindi hicho ilionekana ni wimbo tu wa kumtusi na kumfedhehesha adui wao huyo, lakini kwa tafiti za miaka ya karibuni zimeonesha kuwa na ukweli katika hilo.
Mwaka 1923 Hitler aliwahi kukamatwa, na alifanyiwa vipimo ambapo baadhi ya nyaraka za majibu yake zilipatikana katika jimbo la Bavaria, na Chuo cha Erlangen.
Profesa wa Historia, Peter Fleischmann ambae ndie aliyeongoza uvumbuzi huo wa nyaraka hizo, anafafanua kuwa, wakati Hitler akiwa katika gereza la Landsberg, alifanyiwa vipimo na Dr Josef Brinsteiner ambapo majibu yalionesha Hitler alikuwa na ugonjwa wa "right-side chryptorchidism" Kwa lugha rahisi tu ni kuwa alikuwa hana Korodani ya kulia.
Kwa kawaida, Hasa kwa watoto wa kiume Korodani huwa na kawaida ya kuingia sana ndani, lakini namna anavyokuwa ndivyo huwa zinazidi kujitokeza.
Hivyo tatizo hilo la Hitler linaweza kuwa lilijitokeza tangu akiwa mdogo, lakini bado shahidi nyingi juu ya suala hilo halijathibitishwa vizuri.....!

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages