Miaka 2300 iliyopita, makundi ya panya, nyoka na wadudu walikimbia mji wa kiGiriki wa Helike, baada ya wanyama hawa kukimbia, tetemeko kubwa la ardhi likatokea na mji wote wa Helike ukaharibiwa...
Kutoka hapo, vizazi mbalimbali vya wanaSayansi vimetumia njia kadha wa kadha kujaribu kubashiri matetemeko ya ardhi.
Njia zilizopo sasa ni kama: kuchunguza tabia za wanyama, kuangalia mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na seismogramu... lakini vyote hivyo havijaweza kutoa njia ya uhakika ya kubashiri matetemeko ya ardhi.
Ndoto tuliyonayo ni kufika mahali tuweze kubashiri matetemeko ya ardhi pamoja na ukubwa wake kama tunavyoweza kubashiri hali ya hewa sasa. Kwani tukiweza kufanya hivyo, hata likitolewa tangazo muda mfupi kabla ya tetemeko, linatosha kuwasaidia watu wanaokaa maeneo husika kukimbia mbali na majengo na kuta na kuokoa maisha yao, au hata mitambo ya hatari kama ya nyuklia kuzimwa, ili kuepusha ajali, kama ile iliyotokea Japan. Na kama tangazo likitolewa siku kadhaa kabla, latosha kusaidia watu kuondoka kabisa kutoka eneo husika.
WanaSayansi mpaka sasa wamekuwa wakitumia Seismologia kama njia ya kubashiri matetemeko. Njia hii huangalia matetemeko madogo madogo chini ya ardhi ili kubashiri tetemeko kubwa, lakini mpaka sasa haijawa njia ya uhakika kubashiri matetemeko, na inaleta kazi katika kutofautisha tetemeko kubwa na dogo ambalo halina dhara lolote.
"Mpaka sasa, wanaSeismologia hawawezi kukupa jibu la uhakika la Ndiyo au Hapana, kama kutakuwa na tetemeko kubwa la ardhi mbele." ni maneno aliyoongea Thomas Jordan ambaye ni mkurugenzi wa "Southern California Earthquake Center" katika mkutano wa "American Geophysical Union" (AGU) uliofanyika San Fransisco mwezi uliopita....
Kutokana na hilo, wanaSayansi wengine wameamua kugeuza mtazamo wao, na kuangalia/ kutafuta njia nyingine mbadala, na za uhakika za kubashiri matetemeko ya ardhi... Njia moja ambayo inaangaliwa kwa ukaribu ni "umeme"...
Radi ya Chini ya Ardhi:
Nadharia moja iliyopo ni kwamba: Tetemeko linapotaka kutokea, miamba inayosababisha hutoa umeme mkubwa kama radi.
Tom Bleier ambaye ni injinia, anasema: "Umeme unaotolewa na matetemeko makubwa ni mkubwa sana... kama ampere 100,000 kwa tetemeko la magnitudi 6, na ampere 1,000,000 kwa tetemeko la magnitudi 7, ambayo ni kama radi; sema tu inatokea chini ya ardhi..."
Kupima umeme huu, Bleier na timu yake wametumia mamilioni ya madola kuweka vifaa viitwavyo magnetometea chini ya ardhi katika mistari ya "fault" California, Peru, Taiwan na Greece... vifaa hivi viko sensitive kupima current hizo za umeme...
(For more info, visit the link:
http://news.nationalgeographic.com/
news/2013/01/04-earthquakees-defy-prediction-efforts/ )
WANASAYANSI WATAFUTA NJIA YA UHAKIKA YA KUTABIRI/ KUBASHIRI MATETEMEKO YA ARDHI...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment