USHAHIDI WA NYOTAMKIA (COMET) ILIYOINGIA NA KULIPUKA DUNIANI.


Kumekuwa na Nadharia kwamba, mamilioni ya miaka iliyopita kuna Nyotamkia/Kometi iliyoingia katika angahewa la Dunia na kulipuka; hali iliyofanya wanyama wengi waangamie na kutoweka kabisa.
Pamoja na kwamba nadharia hiyo imekubalika kwa muda mrefu sasa, bado hakukuwa na ushahidi wa hakika kuhusu tukio hilo la Nyotamkia kuingia Duniani kutokea.
Lakini sasa, Timu ya WanaSayansi kutoka Afrika Kusini wakishirikiana na wataalamu wengine, wanaamini wamegundua Ushahidi wa tukio hilo kutokea.
Ugunduzi huo umetoa si tu Ushahidi wa Nyotamkia kulipuka Duniani mamilioni ya miaka iliyopita, bali pia wanaamini unaweza ukatupa mwangaza fulani katika kujua namna Mfumo wetu wa Jua ulivyoanza kuundwa.
Nyotamkia hiyo iliingia katika Angahewa ya Dunia takribani miaka milioni 28 iliyopita, na ilitua ambapo sasa ipo nchi ya Misri (Egypt).
Ilipoingia tu katika angahewa la Dunia ikalipuka mlipuko mkubwa, na kusababisha ardhi kufikia joto la nyuzijoto 2000 °C, hali iliyosababishwa kuundwa kwa glasi ya Silica iliyosambaa katika jangwa la Sahara.
Timu hii ya wanaSayansi ilichunguza jiwe jeusi lililopatikana nchini Misri, ambalo awali lilidhaniwa kuwa ni sehemu ya Kimondo kilichoanguka, lakini baada ya uchunguzi wa karibu zaidi na timu hii; wamefikia hitimisho kwamba jiwe hilo ni sehemu ya Nyotamkia hiyo iliyoanguka mamilioni ya miaka iliyopita.
Ugunduzi huu umepokewa vizuri, kwani unatilia mkazo Nadhari ambayo wanaSayansi wengi wameikubali kwa muda mrefu, Kwamba: Kuna kipindi mamilioni ya miaka iliyopita ambapo Nyotamkia iliingia katika Angahewa la Dunia na kulipuka... Hali iliyofanya Viumbe wengi kutokomea kutoka Uso wa Dunia.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages