TAA ISIYOHITAJI MAFUTA WALA UMEME...


Kuizungumzia taa isiyohitaji mafuta wala umeme wa aina yoyote na inayogharimu dola 5 (Tsh. 7,500) kwa jana ingeweza kuwa ndoto isiyoweza kutimia, lakini si hivyo leo.
WanaSayansi wawili Uingereza wameweza kuifanikisha ndoto hiyo kutimia kwa kutengeneza taa hiyo, yenye jina "GravityLight".
Idea ya kuitengeneza taa hiyo ilikuja ili kutoa njia rahisi na isiyo ya gharama kwa watu waishiyo katika mazingira magumu kupata mwanga majumbani mwao. Lakini wakiwa na ndoto vilevile za baadaye kutoa njia mbadala ya ku-charge simu na redio.
Martin Riddiford na Jim Reeves wametumia muda wa takribani miaka minne kuitengeneza hiyo "GravityLight" ambayo inatumia graviti ya dunia kutengeneza umeme wa kutosha kuiwasha taa hiyo. Haiihitaji betri wala generator...
Ili kuitumia "GravityLight", all you need to do: ni kuitoa kwenye box lake, kuitundika juu, kulijaza begi lake na uzito wowote (mawe, mchanga) wa kilo tisa na kuliacha likining'inia chini ya taa hiyo kwa muda kidogo, na taa inawaka kwa zaidi ya nusu saa. ikififia, unalirudishia tena hilo begi lenye uzito...
Lengo la wanaSayansi hao ni ku-provide mwanga safi, na wa uhakika kwa watu zaidi ya bilioni 1.5 duniani ambao bado hawana uwezo wa ku-afford umeme, na wanatumia taa za chemli ambazo zina madhara ya kiafya...
Kwa sasa, watatoa taa zaidi ya 1,000 kwa vijiji kadhaa Afrika, na kwa kuangalia mafanikio yake au mapungufu, wataanza mass production kwa kusaidiwa na NGO mbalimbali...
Nadhani hii itatufaa hata hapa Tanzagiza...
Waweza kucheki video, kwa kutembelea link ifuatayo:
http://www.youtube.com/watch?v=1dd9NIlhvlI

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages