SAYARI ZA MSHTARII (JUPITER) NA ZOHALI (SATURN) ZAWEZA KUWA NA ALMASI TELE!


Kundi la wanaSayansi likiongozwa na bwana Kevin Baines kutoka chuo kikuu cha Wisconsin-Madison wamesema kuwa: kutokana na tafiti zao; Sayari mbili jitu za gesi zilizo kwenye mfumo wetu wa Jua (yaani Mshtarii na Zohali), zina mazingira yanayoruhusu kuzalisha madini ya Almasi (Diamonds) kwa wingi mno.
Kwa makadirio wamesema, zinazalisha tani elfu moja (1,000) za Almasi kila mwaka.
Namna zinavyozalisha:
Radi kubwa hupiga katika angahewa za sayari hizi za gesi; hali inayofanya molekyuli za methane kugeuzwa kuwa Kaboni (Carbon).
Kaboni hii iliyo katika mfumo wa masizi (soot), huanza kuzama ndani ya matabaka ya gesi za sayari, na kadiri inavyozidi kuzama huanza kukandamizwa na pressure. Mkandamizo huu hubadilisha masizi kuwa graphite na hatimaye kuwa Almasi (Solid diamonds)

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages