NYOTAMKIA/KOMETI (COMET)


Nyotamkia ni gimba dogo la angani linalozunguka jua kwa njia ya duaradufu.
Kometi nyingi ziko mbali na jua... umbali unaozidi orbiti ya sayari ya Neptune.
Pale Kometi inapokaribia Jua, huongezeka joto na kuanza kutoa gesi/mvuke, ambao ukiangalia kutoka mbali waweza dhani imeotesha "mkia", Hali hii ndio unaoipa jina lake la "nyota yenye mkia".
Nyotamkia imeundwa na mchanganyiko wa: mawe (rocks), vumbi (dust) na barafu (ice).
Kama nilivyosema awali: Muda mwingi nyotamkia iko mbali na jua, ikifuata njia ya mzunguko (orbit). Ila, ikikaribia Jua kiasi cha kutosha, huanza kuonekana kama nyota ikiakisi nuru ya Jua.
Ikikaribia Jua zaidi; sehemu ya barafu yake inaanza kuyeyuka kuwa mvuke unaoachana na nyotamkia, na kisha kuonekana kama "mkia".
Mkia huu huelekea kila wakati upande usio wa jua; hii ni kutokana na upepo wa jua (Solar wind) unaopuliza nyotamkia
TOFAUTI KATI YA KOMETI NA ASTEROIDI:
Imewapa wanaSayansi wakati mgumu kidogo kutofautisha kati ya Kometi na Asteroidi; kwani zinalingana kwa mambo mengi.
Lakini, Tofauti kubwa kati ya Kometi na Asteroidi ni muundo wao. Kama nilivyosema awali: Kometi imeundwa na mchanganyiko wa mawe, vumbi na barafu; lakini Asteroidi zimeundwa na madini kama chuma pamoja na mawe.
Jambo la msingi kujua: magimba yote ya aina hizo mbili (Kometi na Asteroidi) yaliundwa mwanzo kabisa wa mfumo wetu wa Jua (miaka bilioni 4.5 iliyopita).
Asteroidi ziliundwa karibu kidogo na Jua, lakini Kometi zikaundwa mbali na Jua, na ndio maana zina barafu.
Tofauti nyingine ndo hiyo kwamba: Kometi zina "mikia", lakini Asteroidi hazina.
Jambo jingine ambalo tunaweza tukaita tofauti ni kwamba: Mpaka sasa kuna mamilioni ya Asteroidi yanayotambulika, lakini mpaka ilipofikia Juni ya mwaka huu, ni Kometi 4,894 tu ndizo zinafahamika.
Nyotamkia/Kometi moja ambayo ni maarufu duniani ni ile inayoitwa "Halley". Kometi hii ilitambuliwa mwaka 1705, na mwanaSayansi wa kiIngereza anayeitwa Edmond Halley.
Jambo jingine pia la kufahamu ni kwamba: Kwa muda mrefu Duniani, watu wamekuwa na imani kwamba Kometi inapoonekana angani, hubashiria kitu kikubwa na kibaya kitatokea... Lakini hizo ni imani tu...
Kwangu mimi; Kometi hunivutia kila inapoonekana, kwani ni jambo la Ki-pekee linalotokea mara chache (kwa kukadiria: Huonekana angani kama mara moja kila baada ya miaka kumi)...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages