NYOTA (STARS)!


Nyota, kwa lugha ya kawaida ni nuru ndogo zinazoonekana angani wakati wa Usiku...
Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisayansi (telescopes), imegunduliwa ya kwamba: Nyota ni magimba makubwa sana katika anga la nje (space) yanayong'aa kwasababu yanatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za mnurunisho kutokana na myeyungano ya kinyuklia (nuclear reactions) ndani yao.
Lakini ziko mbali sana, na ndio maana tunaziona kama nukta ndogo za nuru.
ASTRONOMIA:
Habari za nyota zinakusanywa na kufanyiwa utafiti na sayansi ya astronomia (astronomy). Wanaastronomia (astronomers) wanatumia vifaa kama darubini (telescopes) kutazama nyota na kupima nuru yao.
Kwa kutumia mbinu za sayansi ya Fizikia (Physics) inawezekana kutambua tabia nyingi za nyota ingawa ziko mbali sana.
ASTRONOMIA VS UNAJIMU:
Usichanganye astronomia (astronomy) na unajimu (astrology). Unajimu wenyewe hutumia mbinu za kale sana, lakini HAUFUATI utaratibu wa kisayansi. Unajimu hujaribu kutabiri mambo yajayo kutokana na nyendo za nyota
IDADI:
Nyota zinazoonekana kwa macho wakati wa usiku ni kama 6,000 lakini idadi yao halis ni kubwa zaidi. Hakuna aliyeweza kuhesabu nyote zote. kuna makadirio ya nyuma kuwa idadi inaweza kufika 70,000,000,000,000,000,000,000...
GALAKSI:
Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kundi kama hili huitwa galaksi (galaxy). Galaksi yetu ikiwemo mfumo wa jua letu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Tunaona sehemu za nyota zake angani zikionekana kama kanda la kung'aa linalojulikana kwa jina njia nyeupe (milky way).
MAISHA YA NYOTA:
Fizikia na astronomia zimegundua ya kwamba nyota hazidumu milele bali zina mwanzo na pia mwisho. Kutokana na tabia hii wataalamu mara nyingi huongea juu ya "maisha", "kuzaliwa" na "kufa" kwa nyota ingawa si viumbehai.
Nyota zinaanzishwa katika nebula au katika mawingu makubwa ya gesi kwenye anga la ulimwengu. Kama wingu ambalo sehemu kuwa yake ni hidrojeni ni kubwa sana inaanza kujikaza kutokana na graviti yake. Katika muda wa miaka milioni 10-15 wingu linajikaza kuwa tufe kadhaa kubwa na ndani ya tufe hizi halijoto inazidi kupanda. Kadiri jinsi gesi inajikaza nguvu ya graviti ndani yake inaongezeka na atomi zake zinaanza kugusana. Halijoto inazidi hadi kufikia kiwango ambako mmenyuko mfululizo wa kinyuklia unaanza kutokea hadi kufikia mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kugeukia heli.
Kipindi cha mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kinaendelea kwa miaka mabilioni hadi sehemu kubwa ya hidrojeni imekwisha. Hapa sehemu za nje ya nyota hupoa na kupanuka; halii hii huitwa pandikizi nyekundu (red giant) kwa sababu ya ukubwa na rangi yake. Mapandikizi mekundu kadhaa huonekana kwa macho tu angani yaking'aa kwa nuru nyekundu. Kama masi ya nyota bado ni kubwa mmeyungano nyuklia unaendelea kuzaa elementi nzito zaidi kwa sababu sehemu ya heli inaendelea kujibadilisha kuwa elementi za juu zaidi. Inaaminmiwa ya kwamba elementi zote ulimwenguni zilianzishwa ndani ya nyota.
Mwishowe kama masi haitoshi tena kuendeleza mmeyungano masi inaweza kujikaza; kutegemeana na ukubwa wa masi nyota inaweza kupasuka (supernova). Mabaki ya mlipuko huu yanakaa angani tu na mara nyingi huingia tena katika mwendo wa kuzaa nyota mpya; sehemu ndogo za masi hii huwa sayari.
(mmh. Kiswahili kigumu aisee!
Natumai nimeeleza kwa ufasaha...)

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages