Mpango wa NASA wa kudaka Asteroidi


Kulikuwa na tetesi hivi karibuni, na sasa zinaonekana kuwa sahihi.
Dola milioni mia moja zimetengwa katika bajeti ya NASA kwa ajili ya mpango wake wa kutuma chombo cha kiroboti cha anga (robotic spaceship) kudaka/
kukamata Asteroidi ndogo ya futi 25 (mita 7) yenye uzito wa takribani tani 500, kuibeba na kwenda kuitua kwenye mwezi ili wanaAstronati waweze kuisoma (kuifanyia utafiti zaidi). Mpango huu unategemea kutekelezwa ifikapo mwaka 2019.
Mpango huu, utasaidia kuharakisha mchakato na ajenda ya Marekani hivi sasa ya kuhakikisha wanamuweka/
wanamtua mwanaAstronati wao wa kwanza kwenye moja ya Asteroidi kubwa ifikapo mwaka 2025, na hatimaye kufika Mars kabisa.
Mpango huo wa kulidaka Asteroidi hilo unaonyesha umakini wa Marekani, pamoja na NASA katika kukabili changamoto ya Asteroidi zinazoweza kutua Duniani na kuleta majanga makubwa...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages