MJI WA MASDAR


Mji wa Masdar ni mji mpya unaojengwa Abu Dhabi, UAE.Mji huu ni project iliyo chini ya 'Abu Dhabi Future Energy Company'.
Nia ya ya project hii ni: Kujenga mji wa Kisasa kuliko ile iliyopo sasa, mji ambao utategemea kwa asilimia mia moja nguvu itokanayo na jua (Solar Energy) pamoja na Nishati mbadala (renewable Energy) isiyochafua hewa.
Mji huu vilevile hautakuwa na magari kama haya tunayotumia sasa, ambayo hutoa gesi ya Kaboni inayochafua hewa. Magari ya mji huu yatatumia nishati mbadala, na vilevile yatatembea maeneo yake maalumu, ili kuachia eneo kubwa la watembea kwa miguu...
Mji huu ulianzwa kujengwa rasmi mwaka 2008, na utakuwa tayari ifikapo mwaka 2020, na umegharimu zaidi ya dola bilioni 22 za ki-Marekani.
Mji huu Utakuwa nyumbani kwa watu wapatao 45,000 mpaka 50,000, pamoja na biashara kama 1,500.
Mji huu ni kama picha ya namna miji ya kesho (future) itakavyokuwa. Mji huu umebuniwa na Kampuni ya Kiingereza iitwayo 'Foster and Partners'
(waweza cheki video hii for more info and clear picture:
http://www.youtube.com/watch?v=FyghLnbp20U )

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages