MASHIMO MEUSI (BLACK HOLES)


Shimo jeusi la angani (black hole) hujitengeneza pale nyota kubwa inapoanza kuishiwa mafuta na kukandamizwa kwa graviti yake yenyewe.
Nyota hii hukandamizwa mno na kuwa ndogo mno hata kiasi cha kufanana na gololi...
Kujaa kwa maada (mass) katika ujazo huo mdogo unalipa shimo jeusi nguvu ya ajabu: Nguvu ya uvutano kubwa sana yenye uwezo wa kumeza hata mwanga ukilikaribia ukaribu sana!
Eneo hili lazungukwa na upeo usioonekana lakini mipaka ya upeo huu ni kama mstari ambao kila kitu kinachoupita hakiwezi kurudi tena kwa sababu kinavutwa mno na graviti ya shimo jeusi. Eneo hili laitwa "jeusi" kwa sababu nuru yote inayofika upeo huu inamezwa kabisa hakuna inayorudishwa tena.
Kuzunguka mzingo wa ukanda wa hatari, kitu chochote kabla ya kuzama moja kwa moja katika shimo jeusi huko angani, huvutwa katika spidi ya kasi sana.
Kitu hicho kilichopo katika spidi ya kasi hutoa miale ya X-ray, ambayo wanaAnga huweza kuichunguza kwa kutumia darubini maalum zilizopo angani.
Mashimo meusi humeza kila kitu kilicho mbele yake (mpaka nyota nyingine)...
Mashimo meusi yana sifa mbaya kutokana na sifa yake ya kumeza kila kitu ndani yake na kuvipoteza moja kwa moja. Sifa nyingine ambayo haijulikani sana ni kwamba yana uwezo wa kutengeneza milipuko na kutupa vitu kwa nje. Wanaastronomia wameweza kugundua milipuko ya aina hii miwili ambayo yote imeweza kuvunja rekodi!
Galaksi nyingi zina mashimo meusi katika viini vyake, ikiwemo galaksi yetu ya "Njia Nyeupe" (Milky Way). Mashimo haya meusi yanaweza kuwa na uzito zaidi ya mara millioni ya ule wa Jua letu, ambao umekandamizwa katika duara dogo.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages