Maryam Mirzakhani, ambaye kwa sasa ni Profesa katika chuo cha Stanford, nchini Marekani amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda Tuzo ya Fields Medal; ambayo inachukuliwa na wengi kama Tuzo ya Nobel katika field ya Hisabati (Mathematics).
Tuzo ya 'Fields Medal' kwa ufupi, ambayo jina lake kwa kirefu ni 'International Medal for Outstanding Discoveries in Mathematics' ni tuzo ambayo hutolewa kila baada ya miaka minne kwa wanaHisabati wawili, watatu au hata wanne ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika field hiyo.
Tuzo hiyo hutambulika kama tuzo ya Heshima na kubwa kabisa ambayo mwanaHisabati yeyote aweza pokea.
Tuzo hiyo ilianza kutolewa mwaka 1936, ambapo mwanaHisabati kutoka Finland, Lars Ahlfors aliichukua. Kuanzia mwaka 2006, Tuzo hiyo imekuwa ikiiambatana na pesa taslimu; kiasi cha dola za ki-Canada $15,000.
Tuzo hiyo imekuwa ikibebwa na wanaume tu, tangu kuanzishwa kwake, lakini kwa mara ya kwanza; tuzo hiyo imechukuliwa mwaka huu na mwanamke.
Maryam Mirzakhani ameipata tuzo hiyo kutokana na kazi yake, iliyoongeza ufahamu zaidi katika kuelewa 'symmetry of curved surfaces', pamoja na topiki nyingine kama 'Teichmuller theory', 'Hyperbolic Geometry', 'Ergodic Theory' pamoja na 'Symplectic Geometry'.
Maryam alizaliwa mwaka 1977, Tehran nchini Iran. Alipata Shahada yake ya kwanza ya 'BSc in Mathematics' mwaka 1999 kutoka chuo cha 'Sharif University of Technlogy' kilichopo jijini Tehran. Alijiendeleza kimasoma na kuchukua Shahada ya Uzamifu (PhD) kutoka 'Harvard University' nchini Marekani, na kwa sasa ni Profesa wa Hisabati kwenye chuo cha 'Princeton University' ambacho ni moja kati vyuo mashuhuri nchini humo.
Katika mahojiano, baada ya kushinda tuzo hiyo, Maryam anasema: "Ntafurahi sana kama tuzo hii niliyoshinda itawapa hamasa mabinti wadogo wanaopenda Sayansi na Hisabati. Na natumai kwamba katika miaka ijayo kutakuwa na wanawake wengi wanaoshinda tuzo hii..."
MARYAM MIRZAKHANI, MWANAMKE WA KWANZA KUSHINDA TUZO YA FIELDS MEDAL.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment