MAMBO 15 YA KUJUA KUHUSU UBONGO WAKO...


Ni jambo la kushangaza kwamba bado tunajua kidogo sana kuhusu kiungo kinachoongoza karibu kila shughuli tunayoifanya.
Bado tunaendelea kuutafiti ili kujua namna Ubongo huo unaweza ukaongoza shughuli za viungo vingine, mawazo, hisia na shughuli nyingine nyingi.
Mpaka sasa, vitu vingi havijajulikana kwa undani zaidi, lakini ni swala la muda tu kabla hatujaweza kuutambua Ubongo wa asilimia 100 namna ufanyavyo kazi...
Anyways, yafuatayo ni mambo 15, ya kufahamu kuhusu Ubongo (unaweza ukawa unayafahamu mengine, lakini mengine ukayasikia kwa mara ya kwanza):
1. Ubongo umegawanyika katika sehemu tatu:
- UbongoMbele (ForeBrain): Huhusika na mawazo, hisia, akili, njaa pamoja na mifumo ya mwendo.
- UbongoKati (Midbrain): Huhusika na usikiaji pamoja na uonaji.
- UbongoNyuma (Hindbrain): Unadhibiti utendaji wa mifumo mingine ya ubongo ili kuzifanya sahihi zaidi.
2. Ubongo tena, umegawanywa zaidi sehemu mbili.
- Upande wa Kushoto: Huhusika na mawazo ya uchambuzi.
- Upande wa Kulia: Huhusika na mawazo ya Ubunifu.
3. Si kweli kwamba eti tunatumia asilimia 10 (10 %) tu ya ubongo wetu. Hizo ni stori tu.
Kila sehemu ya Ubongo ina kazi maalum, na muda mwingi huwa bize.
4. Ubongo wako una mishipa ya damu, ambayo ikikunjuliwa (kwa pamoja) ina urefu wa maili 100,000 (urefu unaotosha kuizunguka dunia nzima mara nne)
5. Ubongo wako vilevile una niuroni bilioni 100.
6. Unapojifunza lugha mpya kabla ya kufikisha miaka mitano, Ubongo wako unakua tofauti na watu wengine.
7. Kama Ubongo ungekuwa "hard drive" ya computer, una uwezo wa kutunza kumbukumbu ya hadi terabyte 4.
8. Bingwa wa kumbukumbu duniani, anaitwa Ben Pridmore. Ana uwezo wa kukariri karata zote kwenye box (52) ndani ya sekunde 26.38.
9. Unachokula kinaathiri kwa namna moja ama nyingine Ubongo wako.
10. Asilimia 20 (20%) ya oksijeni unayovuta inatumiwa na Ubongo.
11. Ukubwa wa Ubongo SIO akili nyingi.
Mfano: Ubongo wa kawaida wa binadamu una angalau gramu 1,360. Lakini Ubongo wa Albert Einstein una gramu 1,230.
12. Kuhusu Ubongo wa Einstein, baada ya kufariki, wanaSayansi waliuchukua Ubongo wake, na mpaka sasa umetunzwa ili kufanyiwa tafiti.
(Einstein mwenyewe alikuwa radhi ubongo wake kufanyiwa tafiti akifa, usije ukahofu Ubongo wako utachukuliwa... hahahaha)
13. Wanaume, hutumia zaidi Ubongo wa Kushoto katika shughuli za kufikiri na kuchukua maamuzi. Wanawake hutumia pande zote za Ubongo.
14. Kuna ukweli nyuma ya usemi kwamba: "Wanaume hutumia akili, wanawake hutumia moyo..."
Wanawake hutumia moyo (hisia) zaidi kwasababu wana "Limbic system" kubwa amabayo kazi yake ni kuongoza hisia.
Wanaume wana "inferior-parietal lobule" kubwa ambayo hu-deal na uchambuzi kama Hesabu...
15. Mara kadhaa, mambo huenda kushoto kwenye Ubongo, na error kadhaa zaweza jitokeza... Baadhi ni:
a. "Exploding Head Syndrome": Mhusika husikia milio mikubwa ya kuumiza ikitoka ndani ya kichwa.
b. "Phantom Extra Limb Syndrome": Mhusika hudhani ana mikono zaidi ya ile aliyonayo.
c. "Sleep Paralysis": Mhusika hushindwa kunyanyua miguu yake baada ya kutoka usingizini... Hii ni kwasababu Ubongo bado upo kwenye "REM" mode...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages