Mageuko ya Spishi ni mbadiliko wa tabia za kurithi za viumbehai kadiri vizazi vinavyoendelea.
Mchakato huu huleta mabadiliko mbalimbali kati ya viumbe.
Nadharia hii inategemea kwamba, awali maisha yote yametokana na 'kiumbe' kimoja (ancestor) miaka karibu bilioni 3.8 iliyopita.
Michakato mbalimbali ya Mageuko ya Spishi ndiyo yamepelekea kuwa na viumbe vingi, na vya tofauti kama tunavyoviona leo.
Msingi wa nadhari hii ni mabaki ya kisukuu (fossils) ya viumbehai ambao hawapo tena duniani, lakini wanaofanana kiasi na viumbehai wa leo, pamoja na ulinganifu wa spishi za karibu na mbali zaidi.
VISUKUU (FOSSILS)
Kisukuu ni mabaki ya kiumbehai ama mmea au mnyama kutoka zamani za miaka 10,000 au zaidi. Visukuu vingi vina umri wa miaka mamilioni.
Mabaki haya yanapatikana kwa umbo tofauti, Mfano:
1. Visukuu vya kijiwe.
Mara nyingi miili ya wanyama na mimea imehifadhiwa kwa umbo la jiwe. Ni kama picha au hata sanamu ya kiumbe kile.
Mifano bora imepatikana pale ambako mmea au mwili wa mnyama ilianguka katika matope laini, na kuzama chini haraka. Ndani ya matope laini, mwili haukuoza shauri la uhaba wa oksijeni na uhaba wa bakteria. Polepole maji ya matope yaliingia dani ya mwili na kujaza nafasi zilizojazwa awali na kiowevu cha seli wakati kiumbe kilikuwa hai. Maji ya matope yalipeleka pia minerali mbalimbali ndani ya mwili. Jinsi mwendo huu liweza uendelea polepole bila kuzuiliwa polepole hata seli ziliweza ujazwa kwa vipande vidogo vya matope na minerali nyingine. Kama baada ya miaka mingi matope yalikauka hata matope ndani ya seli za mwili ulikauka lakini wa kutunza umbo la seli hizi. Kama ganda la matope liliendelea kufunikwa na tabaka za udongo wa juu shindikizo la juu lilianza kuibadilisha lile udongo kuwa jiwe na mwamba kabisa.
Sehemu ambako mazingira yalifaa kwa kutokea kwa visukuku huitwa "Lagerstätte" na wataalamu (la-ger-ste-te, neno la kijerumani) na hapa mifano mingi imewahi kuchimbwa. Kutokana na mwendo wa gandunia sehemu hizi zinaweza kupatikana chini ya ardhi au juu mlimani.
2. Visukuu vya Makaa na Mafuta
Sehemu kubwa ya mimea ya kale haikugeukiwa kuwa visikuku vya kijiwe bali mabaki yao yalibadilika wakati yalipokaa kama tabaka juu ya uso wa ardhi yalifunikwa kwa udongo na kubadilishwa kwa shindikizo na joto.
Makaa yote yaliyopo chini ya ardhi ni matokeo ya kazi hii; ndani ya makaa wakati mwingine sehemu za miti bado zinaonekana lakini zimebadilishwa kuwa makaa.
- Kwa njia hii ilitokea mifano kamili ya miili ya spishi zisizopatikana tena duniani. Wataalamu hulinganisha visukuku na wanyama au mimea ya leo na hapo wanapata picha juu ya mabadiliko ya spishi. Nadharia ya mageuko ya spishi iliathiriwa sana na matokeo ya utafiti wa visukuku.
CHARLES DARWIN
Charles Darwin na Alfred Wallace ndio walikuwa wa kwanza kutoa hoja za Kisayansi juu ya Nadharia ya Mageuko ya Spishi inayoendeshwa na uteuzi wa asili (natural selection).
Kanuni zao zilitokana na kweli kuu tatu:
i. Watoto wengi huzaliwa, na wachache huishi/ hustahimili mazingira yao.
ii. Tabia huwa tofauti hata kwa viumbe wa aina moja, hali ambayo huleta utofauti katika kustahimili mazingira na hatimaye kuzaa.
iii. Utofauti huu huweza kurithishwa kwa watoto baadaye.
Kwahiyo; kundi fulani la viumbe linapokufa, kundi jingine lenye tabia tofauti zinazowawezesha kustahimili mazingira yao hudumu, na hivyo uteuzi asilia hutokea...
Kitabu cha Darwin kiitwacho "On the Origin of Species", kinaelezea zaidi na kwa ufasaha mkubwa juu ya uteuzi asilia...
Katika Karne ya ishirini, Sayansi ya Jenetikia imeonesha kwa asilimia kubwa kwamba Darwin alikuwa sahihi sana na nadharia yake.
Kwa mfano; ulingano kati ya viumbe ni mkubwa sana, hali inayoonyesha tumetoka kwa mzazi mmoja (ancestor).
- Tuna ulingano wa KiJenetikia karibu asilimia 98 na makundi ya nyani (apes).
- Tuna ulingano wa KiJenetikia karibu asilimia 85 na panya... n.k
Nadharia hii ni moja ya nadharia zinazopingwa sana kuliko nyingine... na hii ni kutokana na sababu za Kiimani/kidini.
Lakini, Kwa wanaBiolojia na hata Wanasayansi asilimia kubwa nadharia hii ni Kweli kama ambavyo nadharia ya graviti ni Kweli kwa WanaFizikia...
(ntatengeneza albamu, ambayo ntaweka picha kadhaa za visukuu (fossils) ili uone vinavyoonekana)
MAGEUKO YA SPISHI (EVOLUTION):
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment