KWANINI TUNAOTA NDOTO ZA AJABU?


Mara kadhaa, twaweza kuona vitu vya ajabu kweli katika ndoto zetu, ambazo kwa namna moja ama nyingine hazieleweki na hazina maana.
Ndoto hizi zatoka wapi? na zina maana gani?
Kuna baadhi ya stadi zimefanyika ili kujua kwanini hili hutokea.
-> Kuchunguza Watu wenye Amnesia.
Amnesia ni Ugonjwa ambao humfanya mtu kupoteza kumbukumbu zake... Watu waliopoteza kumbukumbu huwa na ndoto za ajabu sana, pengine kuliko hata watu wenye kumbukumbu zao.
Kuna aina mbalimbali za kumbukumbu, na mtu mwenye Amnesia hawezi kutunza baadhi ya kumbukumbu za matukio, ujuzi fulani, facts kadhaa au hata taehe maalum.
Ni ajabu kwamba, katika ndoto: matukio hayo na vitu walivyo visahau vyaweza kuwarudia, hata kama ki-uhalisia walishapoteza kumbukumbu hizo...
Majaribio (experiments) kadhaa yamefanyika, na yameli-prove hilo...
Watu wasio na Amnesia, hata wakiota ndoto za ajabu, mara nyingi huona kitu au vitu wanavyovifahamu, pengine eneo fulani, au hata mtu fulani. Lakini watu wenye Amnesia wakiota ndoto hizo, hawamtambui mtu wala mahala walipo, kwao kila kitu ni kigeni...
Stadi hii imemfanya mwanaSayansi: Dr. Robert Stickgold kutengeneza nadharia ya kwanini ndoto hizi hutokea.
Stickgold anasema: "Watu wenye Amnesia hutunza picha fulani kuhusu tukio husika, na hata kama hawawezi kuikumbuka wakiwa macho... wakiwa wamelala, Ubongo huitoa picha hiyo..."
Katika nadharia yake, Stickgold anaendelea kusema: "Ndoto za ajabu (zisizoeleweka) ni njia ya Ubongo kuchambua signal mbalimbali ili kutafuta mahusiano kati yao."
Kwa mfano: "Ukiota upo kwenye kantini ya shule yenu pamoja na mwalimu wako, umekalia kiti cha chuma, na anatokea waiter kukuhudumia, lakini waiter huyo ni mbwa..."
Kiuhalisia: Ubongo wako umechukua "file" lenye kumbukumbu ya mbwa wako, ikajaribu kuli-compare "file" hilo na "file" jingine ambalo limebeba kumbukumbu ya mwalimu wako ili kuelewa kumbukumbu hizi zinahusianaje...
Kwahiyo, according to Stickgold: Ubongo wako unajaribu kutafuta uhusiano (cross-link)... Mara nyingine uhusiano huu waweza kuwa real, na mara nyingine si kweli...
Stadi nyingine, zimeonesha kwamba: Zile ndoto za ajabu sana zinatokana na activity kubwa katika sehemu ya Ubongo ya "Amygdala ya Kulia" ambayo huhusika na kutengeneza kumbukumbu.
Stadi hii pia, ina-support idea kwamba: "Kadiri ndoto ilivyo ya ajabu (kutoeleweka), Ubongo unapata kazi katika kutafuta uhusiano kati ya kumbukumbu kadhaa..."
Niambie mawazo yako...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages