Geni (genes) za makundi mbalimbali ya nyani (primates) waliopo sasa, zinatuambia kwamba: ukoo wa nyani (ikiwemo binadamu) ulianza kujitenga na makundi ya zamani ya nyani kiwemo sokwe (baboons) miaka milioni 25 mpaka 30 iliyopita.
Lakini, visukuu (fossils) vya makundi yote mawili tulivyokuwa navyo vilikuwa vya miaka milioni 20 tu. Hiyo imebadilika sasa, ambapo kundi la wanaSayansi (paleontologists) wamegundua spishi mpya hapa nchini kwetu Tanzania kwenye Bonde la Rukwa.
(NB: Paleontologists ni wanaSayansi ambao husoma, na kuchimba visukuu.
Kisukuku ni mabaki ya kiumbehai ama mmea au mnyama kutoka zamani za miaka 10,000 au zaidi. Visukuku vingi vina umri wa miaka mamilioni.)
Kisukuu cha kwanza kilifukuliwa mwaka 2011, na kikapewa jina "Nsungwepithecu
s gunnelli". Sasa, kisukuu kingine kimepatikana, na ndicho kikongwe kuliko visukuu vyote vya nyani, na kimepewa jina "Rukwapithecus fleaglei"
Visukuu vyote vilipatikana katika miamba yenye miaka kama milioni 25.2.
Kupata visukuu vikongwe kama hivi huwa ni kazi, kwani huzidi kufukiwa kadiri miaka inavyokwenda...
Timu hii imekuwa ikilisoma na kuchimba bonde hilo kwa miaka kumi sasa...
(Habari zaidi:
http://www.the-scientist.com/?articles.view/articleNo/35555/title/
Oldest-Fossil-of-Ape-Discovered/ )
Kisukuu kikongwe zaidi cha nyani (ape) chagundulika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment