KIMONDO KILICHOTUA RUSSIA CHALETA MAAFA


Kimondo kilichotua Russia juzi, kimesababisha maafa makubwa...
Takribani watu 1,200 wamefikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu kutokana na majeraha yaliyosababishwa na impact ya kimondo hicho...
Mpaka sasa maeneo matatu ambapo vipande vya kimondo hicho vilitua yameshapatikana. Maeneo mawili ni karibu na ziwa Chebarkul, na eneo la tatu lipo umbali wa kilomita 80 kutoka hayo maeneo ya kwanza karibu na mji uitwao Zlatoust.
Kimondo hicho kilichokuwa kikisafiri kwa spidi ya kilomita 30 kwa sekunde (ambayo ni sawa na kilomita 108,000 kwa saa) kilitua chini na kulipuka, na vipande vyake kupasuka na kurushwa kwa mlipuko huo kama bomu.
Maafa yanatokana na vipande hivyo vilivyorushwa, lakini pia kutokana na mlipuko huo, huleta tetemeko la ardhi kwa maeneo ya karibu, na impact yake ni sawasawa na bomu...
Kimondo hicho chenye uzito wa tani 10, kilichoundwa na chuma kiliingia angahewa la Dunia, na kuvunjika vipande kikiwa kilomita 50 juu ya ardhi, na ndo maana kuna eneo zaidi ya moja, ambapo kimetua.
Nguvu (energy) iliyotoka baada ya kimondo hicho kutua ni kilo-tani kadhaa, sawa na bomu dogo la nyuklia...
Katika mji wa Chelyabinsk, nyumba zaidi ya 3,000 ziliharibiwa na tukio hilo pamoja na maafa mengine ya miundombinu.
Mpaka sasa, hakujawa na taarifa yoyote ya vifo vilivyotokana na kimondo hicho...
Taarifa hiyo ya kimondo imekuja muda mfupi baada ya tukio jingine kutokea, ambalo liliwafanya wengi waliolifahamu kusali sala zao za mwisho mwisho (lol), na tukio hilo lilikuwa la Asteroidi moja yenye jina "2012 DA14" lenye diameta ya ukubwa mita 46, kupita karibu na Dunia... na ni gimba pekee la ukubwa wa namna hiyo kufika karibu na Dunia na kutukosakosa katika miaka 15 ambapo wanaSayansi walianza kuchunguza magimba ya namna hiyo...
Kumbuka: Asteroidi ndio iliyoua Dinosauri, kwahiyo waweza kuona uoga nliokuwa nao... hahaha!
(mkipenda naweza ku-post video fupi kuhusu Asteroidi hiyo...)

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages