Kwa muda mrefu, Sayansi imekuwa si kipenzi sana cha watu wengi kutokana na fikra kwamba Sayansi ipo kinyume na Mungu, na ipo pale kumpinga.
WanaSayansi wameonakana kama watu wasio na kazi ya kufanya zaidi ya kumpinga Mungu. Jambo ambalo si kweli.
Sisemi kuwa, hakuna wanaSayansi wasiompinga Mungu. Wapo,lakini nadhani si sahihi, kusimama na kusema kwamba Sayansi ni kinyume cha Mungu, sababu tu ya baadhi ya WanaSayansi.
Ifahamike kuwa wapo wanaSayansi wengi tena maarufu wanaoamini katika Mungu.
Kumekuwa pia na fikra potofu kwamba, wanaSayansi hukaa na kutunga Nadharia ambazo zitakwenda kinyume na Mungu au misingi mbalimbali ya Imani. Jambo ambalo si kweli!
Kwanza, ni muhimu kufahamu tofauti kubwa kati ya pande hizi mbili, yaani Imani, na Sayansi:
Imani hufuata yale ambayo yameandikwa kwenye vitabu vitakatifu kupitia kwa mitume au watu wengine wa Mungu.
Lakini, Sayansi, hufuata 'facts' bila kuangalia watu huamini nini katika hilo; Hutumia njia ya kufanya majaribi (experiments) ili kugundua ukweli wa mambo.
Sayansi hubadilika mara kwa mara, nikimaanisha: Kama wanaSayansi wanafahamu kitu fulani leo, na kesho ukaja ushahidi mwingine mkubwa zaidi kuliko ule wa jana, basi Sayansi hubadilisha ufahamu ule, na ku-adapt kwa huu ufahamu mpya -- Hivi ndivyo Sayansi ilivyo-function kwa miaka mingi...
Sayansi kwa muda mrefu imekuwa ikipigwa vita kwasababu, ilionekana kwenda kinyume na mitazamo fulani ya watu.
Kwa mfano: Zamani watu walidhani kwamba Dunia ndio kila kitu katika Ulimwengu, na nyota zote zinaizunguka Dunia kwasababu ya mistari kadhaa katika vitabu vitakatifu, lakini Sayansi ilipofika mahali na kusema: "Si Kweli!" Dunia yazunguka Jua; wanaSayansi walionekana kuwa wahaini na watu wanaokufuru... (Lakini, leo mimi na wewe twajua nani alikuwa mkweli).
Galileo Galilei (mwanaAstronomia) alifungwa na kanisa la Roma kwa vile tu tafiti zake zilionyesha Dunia huzunguka Jua, jambo ambalo kwa wakati huo lilionekana kama Kufuru.
Hakuna Nadharia ambazo zimeshambuliwa sana katika Sayansi kama Nadharia za "Evolution", pamoja na "Big Bang".
Nadhani ninaelewa kwanini nadharia hizi zimeshambuliwa hivyo, nayo ni kwasababu zinaenda kinyume kabisa na misingi ambayo wengi tumekuwa tukiiamini kuwa ni sahihi, na vile vile zinadiriki kujibu moja ya maswali makubwa ambayo wengi hujiuliza, nayo ni: "Sisi ni nani?" na "Tumetoka Wapi?"
Maswali hayo hujibiwa vizuri tu katika Imani mbalimbali, na watu hukua wakiamini hivyo, kwahiyo Sayansi inapokuja na kuleta mtazamo mwingine, sishangai mtu anapochanganyikiwa, na simlaumu anapofika mahali pa kutoamini mitazamo hii kabisa.
Sishangai kwani, hata Darwin mwenyewe alisita kuitoa nadharia ya "Evolution by Natural Selection" kwa miaka mingi akihofu namna ambavyo watu wangeipokea.
Anyways, sitaingia kwenye debate ya whether "Evolution" ni sahihi au la!
Nachopenda kusema ni kwamba: Nadharia nyingi za Sayansi, especially zile zilizodumu kwa muda mrefu kama "Evolution", zimepimwa na kufanyiwa utafiti mwingi... Na unapoona Nadharia ya KiSayansi imedumu kwa muda mrefu, ina maanisha Nadharia hiyo ni Nadharia yenye nguvu isiyoyumba kirahisi...
Na unapoona vilevile kwamba wanaSayansi wengi wanaoheshimika, wanakubali Nadharia fulani, ujue pia kuna ukweli fulani ndani yake... Labda ije kubadilika huko mbele.
Swali gumu linapokuja ni kwamba: Ufanyeje unapoona kwamba mtazamo fulani wa kiSayansi unakwenda kinyume na mtazamo fulani uliokua nao...
Mimi nadhani kwa mtazamo wangu ni: wewe mwenywe ufike mahali pa kuona ni kipi utakipa priority, kama ni Sayansi au mtazamo huo mwingine.
Lakini si sahihi kufika mahali na kupinga Sayansi, kama vile ni kitu kibaya kwa vile tu haiendani na mtazamo wako.
Labda ukitaka kuipinga, basi ipinge kwa kutoa nadharia yako yenye ushahidi wa kiSayansi wa kutosha; sio tu kukaa na kuwarushia matusi wale waliokaa chini na kufikiri...
(Niambie mtazamo wako juu ya hili...)
Je! Sayansi inampinga Mungu?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment