Eris ni sayari kibete (dwarf planet) kubwa kuliko zote katika mfumo wetu wa jua. Umbali wake kutoka Jua ni zaidi ya mara tatu ya umbali wa kutoka Jua mpaka Pluto (karibu maili bilioni 10).
Inaichukua Eris muda wa miaka 557 kuzunguka Jua kwa mzunguko mmoja.
Eris inaizidi Pluto kwa ukubwa wa zaidi ya asilimia 27 (27 %), na ndio maana ilipogunduliwa mara ya kwanza, iliitwa: "sayari ya kumi".
Eris ilionekana mara ya kwanza, mwaka 2003 kwenye kitengo cha uchunguzi wa anga cha Mount Palomar kilichopo California chini ya usimamizi wa Mike Brown, ambaye ni profesa wa Astronomia katika chuo cha "California Institute of Technology", Chad Trujillo pamoja na David Rabinowitz.
Ugunduzi wao ulithibitishwa rasmi Januari ya mwaka 2005, na tangazo kwa umma likatolewa July 29, 2005.
Umuhimu wa Ugunduzi wa Eris:
Ugunduzi wa Eris ulikuwa na umuhimu mkubwa... Si kwamba tu kwasababu wanaSayansi waligundua gimba kubwa linalozunguka Jua lililo mbali, na hata nyuma ya "Kuiper Belt" (Eneo lennye barafu lililo nyuma ya Neptune)...
Umuhimu wa Ugunduzi huu, ni kwamba uliibua mjadala mkubwa katika jamii ya wanaSayansi, na kusababisha IAU (Internationa Astronomical Union) kuipitia tena maana ya neno "Sayari".
WanaSayansi mbalimbali walikuwa wakidai: "Kama Pluto ina hadhi ya kuitwa Sayari, basi na Eris pia iwe sayari." Na tangazo likatolwea Agosti 24, 2006, kwamba: Chini ya IAU, Eris ni 'Sayari Kibete', na si 'Sayari', hivyo kufanya Pluto ishushwe kutoka daraja la 'Sayari', na kuwa 'Sayari Kibete' pamoja na Sayari vibete nyingine, kama: Ceres, Haumea na Makemake...
Kwahiyo, kama Ulikasrishwa na kitendo cha Pluto, kutokuwa Sayari tena... wa kumlaumu ni Eris...
Ijue ERIS!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment