GALAKSI


Galaksi (Galaxy) ni kundi la nyota nyingi zinazoshikamana pamoja katika anga la umlimwengu zikishikwa na graviti yao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100, lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.
Galaksi yetu ikiwemo mfumo wa jua letu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kama njia nyeupe (milky way). Umbo lake unafanana na kisahani ikiwa kipenyo chake ni miaka ya nuru (light years) 100,000 ikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000. Galaksi ya jirani iliyo karibu angani inaitwa Andromeda ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5 .
Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi bilioni inaweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani.
Ifuatayo ni picha ya galaksi yetu (milky way)...

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages