China, leo Imerusha chombo chao cha kwanza Kabisa kwenda mwezini.
Chombo hicho chenye jina "Yutu" kimerushwa kwa kutumia Rocket yao inayoitwa "Chang'e Moon Lander". Safari hiyo ndefu imeanza leo (Jumatatu) saa saba nusu kwa mida ya huko.
Kama Safari hiyo ikienda vizuri bila matatizo, "Chang'e" itatua kwenye ardhi ya Mwezi katikati ya Mwezi huu Desemba.
Chombo hichi kitakuwa cha kwanza kutua kwenye mwezi kwa zaidi ya miaka 37, kwani chombo cha mwisho kutua kwenye mwezi kilitua mwaka 1976, na kilitumwa na wa-Soviet.
Bwana Zhang Zhenzhoung ambaye ni mratibu wa "Xichang Satellite Launch Center" anasema: "Kurushwa kwa Roketi hii ya Chang'e iliyobeba chombo Yutu kwenda mwezini kunaudhihirishia Ulimwengu Uwezo wa nchi Kubwa ya China", akaendelea kusema: "Tushirikiane pamoja katika Utafiti wa Anga na kutimiza ndoto za China" alipokuwa akihojiwa na Chombo cha Televisheni cha CCTV.
Kama nilivyosema awali Chang'e inatarajiwa kutua Mwezini by Desemba 14 au 15, na kuanza kufanya tafiti mbalimbali za Ki-Sayansi kwenye Mwezi.
Mission hii ambayo ni ya kwanza kufanywa na nchi ya China ipo chini ya programu yao inayoitwa "China's Lunar Exploration Program" ambayo inahusisha awamu kuu tatu ambazo ni: 1. Kuuzunguka Mwezi, 2. Kutua kwenye Mwezi, na 3. Kurudisha sampuli za mawe ya Mwezini Duniani ifikapo mwaka 2020.
Awamu ya kwanza ambayo ni Kuuzunguka Mwezi walishaikamilisha pale walipotuma Vyombo vyao vya "Chang'e 1" na "Chang'e 2" mwaka 2007 na 2010...
Na hii sasa ndio Awamu ya pili, ambayo ni" Kutua kwenye mwezi...
CHINA YATUMA CHOMBO CHAO CHA KWANZA KWENDA MWEZINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment