USIPOKUWA TAYARI KULIPA GHARAMA USITEGEMEE MAFANIKIO
Habari ndugu rafiki na jamaa popote ulipo mida hii namatumaini uko salama kabisa hadi wakati huu leo nataka tuzungumzie juu ya kulipia gharama za mafanikio, ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu anahitaji mafanikio, hata ukimuuliza mtu wa aina ganj atakwambia anataka kufanikiwa, anataka kuwa na maisha mazuri na mafanikio makubwa lakini tujiulize ni kweli watu wote wako tayali kulipia gharama za mafanikio? Hapa ndio tatizo linakuja watu wengi wanataka kupata mafanikio lakini hawako tayali kulipia gharama za mafanikio, leo nataka nikukumbushe kitu kama hauko tayali kulipia gharama za mafanikio usitegemee kufanikiwa katika maisha, matajiri wote unaowaona leo walilipia gharama za mafanikio yao hapo nyuma ndio maana leo wanashangilia mafanikio yao.ni gharama gani ambazo unapaswa kuzilipa kabla ya mafanikio yako?
1.PESA
Gharama ya kwanza unayotakiwa kulipa ni pesa siku zote huwezi kuwa unataka kuvuna mahindi halafu ukapanda maharage kama unataka pesa lazima mwanzo uzitoe pesa, matajiri wooote unaowaona leo walilipia pesa kwanza ndio wakapata pesa kesho, walizilipa wapi hizo pesa
》Semina:hebu jiulize mwaka jana umeisha umehudhuria semina ngapi za ujasiriamali au zinazotoa mafundisho ya mafanikio yako? Huenda hujahudhuria hata moja, mwaka mmoja uliopita nilipokuwa na mimi kwenye kundi la watu wanaotaka mafanikio halafu sitaki kulipa gharana nilikuwa nashangaa sana unasikia semina imefanyika marekani kiingilio laki nane naona kama wanapoteza pesa, haya hapa hapa dar eti semina 5000 aaa yani elfu tano semina tu, nikawa naona kama naibiwa tu, daaah nilipogundua kuwa semina moja inaweza kubadilisha maisha yangu, watu walikuwa wanashangaa, mtu ananiletea taarifa ya semina halafu mwisho wa siku ananiambia lakini itabidi ulipie namuuliza bei gani ananiambia 15000, namwambia sawa anadhani sitakwenda, nikienda anashtuka hakujua kama sasa nimetambua kuwa mafanikio lazima ulipie gharama, leo ninaposikia sehem kuna semina ya kubadilisha maisha yangu hata kwa mawazo hata iwe bei gani nitajinyima hata kula ili mradi nikasikilize nijifunze, kwasababu nakumbuka jinsi semina moja ilivyobadilisha maisha yangu.Rafiki usidhani mbinu za mafanikio ziko kwenye muvi au kijiweni, ziko huko kwenye semina za biashara, kama unaona huwezi kulipia siku moja utaendelea kuwaona walioko tayali kulipia gharama wanabadilisha maisha yao we ukibaki hapo.
》Kujisomea vitabu:hahahaaaa hapa ndio ilikuwa mtihani kwangu, nilikuwa napita sehem nakuta kitabu kimeandikwa HOW TO BE RICH napenda lakini kikwazo cha kwanza nauliza bei naambiwa 15000 na vingine 20000 hahahaaa nacheka nafikiria yani hichi kitabu sio cha shule, hupati cheti lakini eti bei hiyo yote mmmmhhh huu wizi, na jikifikiria mtu mwenyewe nikisoma kurasa mbili tu nalala.naona bora hiyo pesa nikaangalie muvi nikanunue vitu vya kutumia hata vingine sio vya msingi.
Daaaah Asante Mungu maaana sijui ningezeeka nikiwa mjinga kiasi gani, hebu jiulize hadi sasa hivi umetoa pesa yako kiasi gani kununua vitabu na kuvisoma kama bado jua bado mafanikio yako yako mbali saaana, maana ubongo wako umezeeka, mtu asiekuwa tayali kujisomea vitabu ni sawa na mzeee wa miaka mia akili yake inarudi utoto.Ngoja nikwambie kitu kama kipo kitu ambacho nakithamini leo ni kununua vitabu na kujisomea, bajeti yangu ya nguo yoooote sasa hivi nimeweka kwenye vitabu, hakika ukiwekeza pesa yako kwenye vitabu unalipia gharama ya mafanikio yako na kamwe hutaweza kuwa masikini.THERE IS KNOW POVERT FOR MAN WHO INVESTING IN HIS MIND AND WILLING TO ACT msemo huo huwa unanitia nguvu sana lakini huwa unanifanya moyo wangu kuwa na simanzi maana najua bado kuna kundi kubwa sana la watanzania huenda ukiwemo na wewe bado wanaamini kununua vitabu vya kujiendeleza ni kupoteza pesa, kamwe hautakuwa masikini kama utaweza kujisomea vitabu.
Ngoja niishie hapo baadae nitakwambia gharama nyingine unazotakiwa kulipia.
RAFIKI KAMA HAUKO TAYALI KULIPIA GHARAMA ZA MAFANIKIO YAKO USITEGEMEE KUFANIKIWA KAMWE.
AMKA SASA
@mr Trevo
No comments:
Post a Comment