Soma hadithi ya kusisimua ukiisoma utaikubalii !!!!!

FACEBOOK CHATTING 1
By Imatheboy
Ngoja nikwambie kitu mshikaji wangu. Hapa duniani kuna mademu wanapenda sana kuwa na mabwana wenye fedha, yaani wao wakiona noti tu, mapigo ya moyo yanawadunda sana.
Ukiachana na hao, pia kuna mademu fulani hivi wanapenda kuwa na masupastaa, yaani mtu ukionekana kwenye kideo au ukiwa unatokeatokea tu kwenye magazeti kwamba umefanya tukio fulani hasa lililokuingizia fedha, basi nao hao wanakuja,k wanataka kukuchukua.
Ngoja nikupe mkasa wangu na mademu fulani hivi. Najua wengi mnanijua kwa jina la kisanii la imatheboyclassic lakini jina langu halisi ni Emmanuel. Mimi ni mwanaharakati ninayetamba sana ambaye kwa kipidi kirefu nimekuwa nikisumbuliwa na watoto wa kike, ukikaa leo, wanakupigia simu, wengine wanataka kukuona huku wengine wakikuuliza unaishi wapi waje kukutembelea.
Usupastaa raha sana, baada ya kutembea na mademu wengi, leo hii ninaamua kukupa stori yangu, niliupata vipi usupastaa ambao umenifanya nitembee na wanawake lukuki Facebook, yeah! Wao si wanataka kuwa na supastaa, basi bila kipingamizi nikatembea naye. Wa kwanza kabisa ambaye ningependa kuanza naye, huyu anaitwa Amina Juma ila kwa Facebook anajiita Precious Ammy.
Siku ya kwanzakwanza naingi facebook, sikuwa supastaa lakini maisha yangu ni ya fedha sana. Kwanza nimezaliwa katika familia yenye fedha, wakati wewe unangaika usiku na mchana kutafuta fedha ili utembelee matako, mwenzako mimi nimezaliwa magari yapo uani, yaani nikiwa na miaka nane, tayari kaka alishaanza kunifundisha kuendesha gari.
Kuhusu fedha, familia yetu ina fedha mno, nakumbuka kipindi cha nyuma kaka alichukua wanawake wengi eti kwa sababu alikuwa akitembelea gari. Wanawake bwana, yaani gari tu, hawataki kujua kama ni lako au umeazima, ili mradi umekaa katika kiti cha dereva basi ‘credit’ zote zinakuja kwako.
Baada ya kujiunga na facebook nikaanza kutafuta mademu. Unajua nini mshikaji wangu, mi nimezaliwa kwenye familia ya wapenda sketi, sijui kwa nini. Yaani kuanzia babu yetu mpaka mimi tumekuwa wazee wa sketi tu, ila katika yote hayo, huwa hatutembei na wake za watu, labda itokee sana ndiyo kidogo tunatembea nao.
Baada ya kujiunga na facebook, nikakutana na warembo wengi sana, wazuri na wanaovutia. Si unajua wapo damuni mwangu bwana, demu wa kwanza ambaye nilivutiwa naye, huyu aliitwa Amina Juma, kama nilivyokwambia kwamba huku Facebook alikuwa akijiita Precious Ammy.
Kabla ya kuanza kumtokea kwa kumchombeza maneno ya hapa na pale, nikaanza kuangalia ‘profile’ lake nione anafananaje kwa picha nyingine, anaishi wapi na kama anasoma, anasoma wapi.
Mtu mzima nikajitosa, kucheki ‘profile; lake, mtoto alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam, nikaona poa, anakaa wapi? Kucheki vizuri, mtoto anapatikana hapahapa Dar, nikasema poa, amekwisha.
Nitamuanzaje sasa? Najua wanawake wanafagilia magari, je natakiwa nimtumie picha huku nikiwa kwenye V8 ya baba au nimtumie picha nikiwa Mlimani City huku pembeni kukiwa na Range SV ya kaka, nikaona kwanza ngoja nivumilie, vitu hivyo atakuja kuviona tu.
MIMI: Habari yako bibie.
Kama kawaida yangu, mimi ni kijana mstaarabu, hivyo nikatoa salamu kiustaarabu. Ila si unajua mademu wa kibongo walivyo, ukitoa salamu, kwanza kukujibu mpaka apende yeye mwenyewe. Nikasikilizia meseji kutoka kwake, holaaaa, mtu mzima nikaona nimepatikana.
Wala sikuchelewa, kwa sababu pepo la michepuko lilishaanza kufanya kazi mwilini mwangu, nikaendelea na mishemishe, kila siku nikawa namtumia Amina meseji lakini akawa kimyaaa. Wala sikuujali sana ukimya wake, nilichokifanya ni kuendelea zaidi huku nikizichukua picha zake na kuziweka katika kompyuta yangu. Eti baada ya mwezi kupita, ndiyo akaja kuijibu salamu yangu.
AMINA: Salama tu.
MIMI: Mbona kimya kirefu jamani, nimekutumia salamu mwezi uliopita ndo unanijibu leo, aiseeeee.
AMINA: Samahani, nilikuwa kwenye mitihani.
MIMI: Kwani unasoma wapi?
Nilimuuliza kimbea tu kwani nilikuwa nikipafahamu alipokuwa akisoma, si alipaandika bwana kwenye profile lake.
AMINA: Nasoma Mlimani.
MIMI: Hongera sana.
Baada ya hapo, hakutuma tena meseji, akauchuna, nikaona sio kesi, si tumekwishaanza bwana, ngoja tu, tutasonga kibishi.
Ngoja nikwambie kuhusu huyu Amina. Ninaposema kwamba huyu manzi alikuwa mkali wewe niamini tu. Mtoto alikuwa mfupimfupi hivi, alikuwa amejazia sana maeneo ya kati. Sura yake, kama kawaida ilikuwa na vishimo mashavuni, kila alipokuwa akionekana, uso wake ulijawa na tabasamu.
Picha zake nyingi alizokuwa ameziweka Facebook zilikuwa ni za mitegomitego tu, maa kapiga klabu akiwa na kisketi kifupi, mara kapiga pembeni ya bwawa la kuogelea akiwa na kinguo cha ndani, yaani kwenye kila picha, alikuwa akionekana kimitego.
Kwa kumwangalia, alionekana kutoka kwenye familia bora kama nilivyokuwa mimi, hivyo sikuwa na wasiwasi kabisa kwani niliamini kwamba tulikutana watu wa aina moja kwani kama yeye alikuwa akikaa Msasani, na mimi ninavyokaa Osterbay, kuna ubaya kwani? Wote si majirani tu, kama kwao nyumba ghorofa, kwetu kulikuwa hivyohivyo, kama kwao kuna magari, basi kwetu ndiyo yamejazna tele, hivyo sikuogopa wala nini.
Amina akurudi tena, alikuwa kimya zaidi, kila nilipokuwa nikijitahidi kumtumia meseji, hakuwa akijibu hali iliyoonesha kwamba alikuwa bize sana mpaka kukosa muda wa kuingia Facebook.
MIMI: Ukimya wako unanitia mashaka.
AMINA: Oooh! Samahani mkaka. Nimesafiri nimekuja huku Morogoro kumtembelea bibi.
MIMI: Waoooo! Mtoto wa bibi huyo. Natamani nije nikutembelee.
AMINA: Unakaribishwa sana.
MIMI: Sawa. Nitakuja, hata ikiwezekana leo hiihii.
AMINA: Utaweza kuja leo hiihii? Muda umekwenda sana, saa moja hii.
MIMI: Hahaha! SI nitatumia usafiri wangu, kuna tatizo kwani?
Kwanza ni lazima ujue kwamba mimi napenda SIFA. Nilikwishaona kwamba kwa mapozi anayoniletea Amina nisingeweza kumpata mpaka pale ambapo ningeanza kujifagilia. Mi si ninajua uchawi wao bwana! Uchawi wa mzungu ndiyo ambao unawafanya wote kuchanganyikiwa, hivyo nilitaka kumpa taarifa kwamba ule uchawi wa mzungu (gari) nilikuwa nalo, hivyo hakutakiwa kuwa na wasiwasi na mimi.
AMINA: Una usafiri?
MIMI: Kadogo tu, ninao ila mbovumbovu.
AMINA: Ahahah! Eti mbovumbovu.
MIMI: Sure. Au mpaka niagize jingine wiki ijayo.
Nilikwishagundua kwamba Amina alikuwa msichana wa kutaka mashauzi hivyo na mimi nilitakiwa kuwa hivyohivyo, picha zake za Facebook zilinifanya kugundua kwamba alikuwa msichana wa aina gani. Picha zake nyingi zilikuwa ni za sehemu ya starehe, hivyo nikaona kwamba piga ua, msichana huyu alikuwa ni wa starehe tu.
AMINA: Mpaka uagize jingine? Wenzako hata hilo bovubovu tunalitaka.
Hahaha! Mademu bwana. Tayari kajisahau. Nilipokuwa nikiangalia picha zake, alikuwa ametupia nyingi huku akiwa kwenye gari la hali ya chini, gari fulani hivi ambayo haizidi hata milioni tano, nyingine aliandika ‘My new ride, let me roll’ ambay nayo alikuwa kwenye gari, kwa harakaharaka lilikuwa na gharama kama milioni tatu. Kumbe inawezekana yale hayakuwa yake.
MIMI: Acha nalo, lishakuwa skrepa. Hivi naweza kukuuliza swali?
AMINA: Niulize tu.
MIMI: Hapa Dar es Salaam unaishi maeneo gani?
AMINA: Naishi Magomeni Mikumi.
Hahaha! Sasa, hivi huyu msichana mbwembwe zote zile kazitoa wapi? Yaani nilifikiri anaishi Masaki, kumbe, loool, alikuwa akiishi Magomeni. Mpaka hapo nikaona kwamba huyu demu hachomoki, piga ua lazima nitamchukua tu. Niliringia utajiri wa baba yangu hivyo niliona kwamba ni lazima nimchukue tu.
Kumbuka kwamba hapo bado sikuwa supastaa, nilikuwa mtu wa kawaida tu japokuwa familia ilikuwa na fedha kinoma.
MIMI: Karibu nyumbani kwetu.
AMINA: Unaishi wapi?
MIMI: Naishi Osterbay.
AMINA: Unaishi Osterbay?
MIMI: Yaap. Lini utakuja kunitembelea jamani?
AMINA: Mmmh! Sijui.
MIMI: AU unaogopa mbwa?
AMINA: Kwani hapo kwenu wapo?
MIMI: Ndiyo, ila hawatokung’ata.
AMINA: Hahha! Kweli?
MIMI: Niamini.
Nilikuwa natumia fursa. Baba yangu ana fedha bwana, sasa kwa nini nisitumie fursa hiyo kukamatia mademu? Nikaona kwamba huondiyo ulikuwa muda muafaka, hivyo nilitakiwa kufanya hivyo kama kawaida yangu.
Kuanzia hapo, mtoto Amina akawa ananitumia sana meseji, si unajua nilimwambia kuhusu uchawi wao bwana kwamba nilikuwa nao. Na mimi sikutaka kuchelewa, hapohapo nikaanza kutupia picha nikiwa mbele ya ‘mkoko’ wangu wa maana, basi daah! Kila mtu aliyeLIKE, na yeye alikuwa mmoja wapo, nikaona yes, kashachinjwa huyu, kwa kutumia mali za baba, angenikomaje.
Baada ya wiki moja, Amina akarudi jijini Dar. Mara baada ya kufika, kitu cha kwanza kabisa akataka kuniona, nikamwambia hakuna noma, tungeonana soon. Baada ya siku mbili, nikamwambia tuonane Chagga Bites kwa ajili ya chakula ha mchana.
Pamoja na mbwembwe zake zote hizo, hakuwa akipafahamu Chagga Bite, nikaona kweli mademu wana visa, yaani pamoja na mashauzi yake, sehemu kadhaa za kula bata hakuwa akizifahamu, nikaanza kumuelekeza weeee, alipopapata, jioni ya siku hiyo akatia timu.
Nakumbuka siku hiyo yeye ndiye alikuwa wa kwanza kufika mahali hapo. Alipokaa, nikamwambia aagize na mimi ningelipia, kweli mtoto akaagiza. Baada ya dakika arobaini, akashtukia kwa mbali gari la kifahari likianza kuegeshwa, mlango ulipofunguliwa, akatoka jamaa mmoja hivi, kwa muonekano alikuwa kama Jay Z, huyo alikuwa mimi, the boy.
Nikaanza kupiga hatua kwenda kule alipokaa, nilipomfikia, nikamgusa begani na kumshika, alipogeuka, akapigwa na mshtuko, kuniangalia, nilikuwa handsome, nanukia, fedha zilinifanya kung’aa sana, akajiona kuwa miongoni mwa wasichana waliokuwa na bahati mno.
AMINA: Karibu imatheboy.
MIMI: Asante. Umependeza (Nilimsifia japokuwa alionekana wa kawaida sana, labda kwa sababu nishazoea kuwaona mademu zetu wa kule Osterbay walivyokuwa wakipendeza)
AMINA: Asante.
Siku hiyo niliongea naye mengi. Alikuwa sana na nililipia gharama zote. Baada ya hapo, nikamchukua na kumuingiza ndani ya gari. Harufu ya manukato aliyokutana nayo garini, akabaki akizichezesha pua zake tu. Mtu mzima nikawasha gari na kuondoka mahali hapo.
Nilipiga naye stori, kwa muonekano tu alijiona kuwa mshindi kupata mwanaume kaka mimi. Wala sikuwa nimemtogoza, nilijua tu kwa advertise zangu ilikuwa ni lazima anipende tu.
Tulipofika Magomeni, nikateremka, nikaelekea katika mashine ta ATM, nikachomoa laki tatu, nikarudi garini na kumgawia lakini mbili na nusu.
MIMI: Hizi zitakusaidia kuweka vocha.
AMINA: Jamani baby, nashukuru sana.
Aliniambia na kunipiga busu.
Nilimshangaa sana, sikuwa nimemtongoza, nilimchukulia kama rafiki japokuwa nilikuwa nimemtamani, eti kidogo tu, tayari alikuwa ameanza kuniita baby. Nani alikuwa baby wake? Mi nilikwenda kwake kitamaa tu na wala hakutakiwa kuniita baby.
Siku hiyo sikuwa na presha, nilichokifanya ni kuondoka na kumpeleka kwao huku nikiwa na uhakika kwamba hachomoki. Kwanza ataanzia wapi?
Demu mrembo, Facebook aijifanya ana hela kumbe mweupe tu, masikini kama masikini wengine, nikaona, huu ni wakati wangu wa kufanya yangu, sikuwa na presha kivile, lengo langu lilikuwa ni kuwatembelea wanawake waliokuwa wakijifanya wazuri Facebook, niliamini nitafanikiwa tu.
Nilipomfikisha kwao, huyooooo, nikasepa zangu huku nikiahidi kuwasiliana naye.
Huo Ndiye Amina. Usiwe na pesha, kuna listi ya mademu wengi inakuja. Kwa kutumia fedha za baba, walinikoma.
Itaendelea.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages